Unguja.Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe
ameyaaga mashindano ya Kombe la Mapinduzi bila kuwa na bao lakini
amesema hatayasahau maajabu aliyoyapata katika mechi zao mbili za
mwisho.
Akizungumza na gazeti hili jana, Tambwe alisema si
jambo geni kwake kupoteza nafasi za kufunga, lakini nafasi ambazo
amezipoteza katika mechi mbili za Yanga dhidi ya Shaba katika hatua ya
makundi na ule wa robo juzi dhidi ya JKU hatayasahau katika maisha yake.
Tambwe alisema hajui nini kilitokea wakati
akimalizia nafasi ambazo alikuwa akizipata uwanjani na hali hiyo
haijawahi kumtokea tangu atue nchini.
إرسال تعليق