Makamanda wa mikoa mitatu Simiyu na shinyanga wavunja ngome hatari ya mtandao wa Ujambazi.

Makamanda wa polisi wa mikoa mitatu ya simiyu, shinyanga na mwanza wamefanikiwa kuvunja mtandao hatari wa ujambazi uliokuwa unaongozwa na mfanyabiashara wa mjini bariadi Njile Samwel huku makachero wa jeshi hilo katika mikoa ya kanda ya ziwa pia wakikamata watuhumiwa watano, bunduki moja ya SMG, risasi 331 na mifupa inayodaiwa kuwa ya binadamu.
Kamanda wa polisi mkoani mwanza, SACP  Valentino Mlowola, akiwa ameambatana na kamanda Justus Kamugisha wa mkoa wa shinyanga pamoja na Charles Mkumbo wa mkoa wa simiyu wanajitokeza kwa waandishi wa habari kuelezea tukio la kukamatwa kwa njile samwel ambaye amekuwa na tabia ya kunzisha mtandao wa uhalifu na kisha kuwaua kama mbinu ya kukwepa wapelelezi.
Kamanda wa polisi mkoa wa simiyu Charles Mkumbo anaeleza namna ambavyo kiongozi huyo mkuu wa mitandao ya ujambazi kanda ya ziwa alivyoweza kumuua mshirika mwenzake wa ujambazi chambalu nkono kwa kutumia silaha aina ya smg iliyokuwa na magazini yenye risasi 40 ndani ya pori la akiba la maswa.
Kuhusu tukio la kutekwa kwa mtoto pendo emanuel mwenye ulemavu wa ngozi wa ngozi lililotokea desemba 27 mwaka jana katika kijiji cha ndami wilayani kwimba., kamanda wa polisi mkoani mwanza valentino mlowola amesema polisi inaendelea kuwashikilia watuhumiwa wanane akiwemo baba mzazi wa mtoto huyo baada ya mchujo kufanyika huku akisema jeshi hilo halitashindwa kumpata mtoto huyo akiwa hai au hata amekufa.

Post a Comment

Previous Post Next Post