Manyika
Peter akijifua na timu yake ya Simba katika Uwanja wa Amaan Zanzibar
walipokuwa wakishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Goli kipa
namba mbili wa klabu ya Simba Manyika Peter, leo amechagulia na Kocha
mkuu wa timu ya Taifa Mart Nooij kujiunga na Timu ya Taifa ya Maboresho
ambayo inakabiliwa na mchezo wa kirafiki na Rwanda hapo January 22 mwaka
huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza.
Mbali na
Manyika pia Kiungo chipukizi wa Yanga Salum Telela amejumuishwa katika
kikosi hicho kwa mara ya kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha juu akiwa
na Klabu yake hiyo ya Jangwani.
Nooij
amesema kuwa Stars wataingia kambini januari 18, ambapo wachezaji 16
watakuwa kambi ya Dar es salaam na wengine 10 wataingia kambi ya Mwanza,
itakapo fika januari 19, Wachezaji wote wa Dar es salaam na Mwanza
wataungana kambini sehemu moja jijini Mwanza tayari kwa mechi januari 22
ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba.
Wachezaji wengine ni Aishi Manula kutoka Azam FC, Benedict Tinoco wa Kagera Sugar na Manyika Peter wote ni makipa.
Mabeki ni
Miraji Adam wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicent wa Mtibwa Sugar, Gadiel
Michael Mbaga wa Azam FC, Emanuel Semwanda wa African Lion, Joram
Mgeveke wa Mwadui, Edward Cherles wa Yanga, Mohamed Hussein wa Simba na
Salum Mbonde wa Mtibwa Sugar.
Viungo ni
Salum Telela wa Yanga, Adam Paulo Salamba wa Bulyankulu SC, Hassan
Banda wa Simba, Said Juma Makapu wa Yanga, Said Hamis Ndemla wa Simba,
Hassan Dilunga wa Yanga, Hussein Moshi Malombe wa Geita Gold SC, Shiza
Ramadhani wa Mtibwa Sugar, Omary Nyenje wa Ndanda FC, pamoja na Alfred
Juma Masumbakenda wa Bulyankuru
Source: hivisasa.co.tz
Post a Comment