MAPAJA YA JACK YAZUA TAFRANI


Stori: Imelda Mtema MAPAJA ya staa wa Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan ‘Jack Maisha Plus’ yamezua tafrani baada ya wanaume wakware kumsimamia na kumshangaa kutokana na kuvaa nguo fupi iliyomuacha mtupu mapajani.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo lililowafanya watu washindwe kuendelea na shughuli zao kwa muda lilitokea juzikati katika mgahawa maarufu wa Cape Town Fish Market uliopo Msasani jijini Dar ambapo staa huyo alipoona watu wanazidi kumkodolea macho, aliamua kutimka.
“Nilikwenda na kustarehe na marafiki zangu ambao nilikuwa siko nao muda mrefu hapa nchini, sasa nikashangaa ghafla watu wamenizunguka wanahangaikahangaika hadi shughuli za watu hotelini hapo zikawa haziendi vizuri, nikatoka nduki,” alisema Jack.

Post a Comment

أحدث أقدم