MASKINI BI. CHEKA: LICHA YA USTAA MAISHA ANAYOISHI YANASIKITISHA!

Mwandawa Khamis, Katibu Mtendaji Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (UWWZ)
Jamii imetakiwa kukubali ushiriki wa watu wenye ulemavu katika shughuli za kisiasa ikiwa ni pamoja na uongozi.
 
Katibu Mtendaji kutoka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (UWWZ), Mwandawa Khamis, alisema watu wenye ulemavu wamekosa ushirikishwaji wakionekana hawana nafasi katika uchaguzi wa kisiasa.
 
Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa siku moja kati ya taasisi yake na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) na UN Women Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
 
Alisema mara nyingi nafasi za uongozi kwa kundi hilo zimekuwa ni za viti maalum, lakini pia huangushwa wakati wa uchaguzi wa ndani ya vyama.
 
Akitoa mfano wa uchaguzi wa mwaka 2010, alisema wanawake 11 wenye ulemavu walijitokeza kugombea nafasi maalum zikiwamo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka jumuiya yake ambapo hakuna aliyeshinda.
 
“Safari hii pia tumejipanga kugombea hadi nafasi za jumla ila sambamba na hilo, tunahitaji jamii ibadilike ili itukubali kuwa wagombea na kutuchagua kutokana na uwezo wetu siyo ulemavu wetu,” alisema.
 
Aliitaja jamii kuwa ni pamoja na wapiga kura katika hatua ya uchaguzi wa ndani ya vyama, wapiga kura wa jumla na zaidi viongozi wa kisiasa.
 
Naye mjumbe wa umoja huo, Saada Hamad Ali, alisema ushiriki wa watu wenye ulemavu ni muhimu ili watetee kundi hilo linalokabiliwa na changamoto nyingi zaidi.
 
Alisema kundi hilo linakabiliwa na ukatili mkubwa wa kijinsia na ambapo kwa asilimia kubwa kesi zake hufelishwa mahakamani.
Akitoa mfano, alisema kwa mwaka 2011 hadi 2014, zaidi ya kesi 115 ziliripotiwa lakini ni kesi mbili tu ndizo zilizopata haki mahakamani.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم