Wastani
wa mshahara nchini Burkina faso ni takriban dola 150 kwa mwezi, kwa
mujibu wa Mbunge kutoka baraza la mpito nchini humo ,mishahara
inahusisha malipo ya vikao vya bunge, malipo ya shughuli za ofisi,
malipo kwa ajili ya huduma za afya na gharama za mafuta.
Lakini
Mratibu kutoka asasi moja ya kiraia ya nchini humo Herve Kam anasema
malipo ya baada ya kuhudhuria bunge hayakupaswa kuwapo akieleza kuwepo
kwa utofauti mkubwa kati ya Maafisa wa serikali na raia wa kawaida.
Tangu
mwezi Oktoba mwaka jana Rais Blaise Compaore alipoondolewa madarakani,
baraza la mpito lilikuwa na wawakilishi 90 ambao waliwakilisha
lililokuwa bunge la nchi hiyo.
Mmoja wa wabunge anaunga mkono
hatua hii ya kupunguza mishahara akisema hatua hii inaimarisha utawala
bora na demokrasia thabiti.
Hali ilikua ya mtafaruku Baada ya
kubainika kwa kiasi cha mishahara ya wabunge hali iliyosababisha
ghadhabu miongoni mwa jamii kupitia kwenye mitandao wakikemea kile
walichodai kutotendewa haki na kutaka viongozi kuacha kutumia madaraka
yao vibaya.
Baada ya kupambana kubadilisha Serikali ya Burkinafaso, raia nchini humo wana matumaini ya kuweka mfumo mpya na mzuri wa haki(BBC)
إرسال تعليق