MWANAMKE
mmoja mke wa mtu anayejulikana kwa jina la Latifa Ally, hivi karibuni
alikamatwa akiwa na hawara yake aitwaye Mose Kessy, wakidaiwa kuiba gari
aina ya Toyota Opa lenye namba za usajili T 818 BHG la John Alex, mkazi
wa Moshi mkoani Kilimanjaro, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.
Alex ambaye ni mume wa Latifa wakiwa na miaka nane katika ndoa yao,
ambaye ni mfanyabiashara wa usafirishaji mizigo, anadaiwa kumnunulia
gari hilo mkewe kama zawadi.
Inadaiwa kuwa baada ya kupewa gari hilo, Latifa alisubiri kwa muda
hadi mumewe aliposafiri kikazi, ndipo alipoondoka na hawara wake huyo,
wakitanua sehemu mbalimbali nchini, ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro na
Tanga.
Akizungumza na mwandishi wetu, Alex alisema alisafiri kikazi kuanzia
Desemba 10-12 mwaka jana, lakini aliporudi alikuta mkewe akiwa ameondoka
na gari lake pamoja na Mose Kessy.
“Baada ya kurudi safari sikumkuta mke wangu kitu ambacho si kawaida
yake, nilianza kufuatilia mawasiliano yake na kubaini kuwa ana mtu
anawasiliana naye kwa Instagram yuko jijini Dar es Salaam na
alitambulika kwa jina la Mose Kessy.”
Kufuatia jambo hilo, Alex alifungua malalamiko katika kituo cha
Polisi Moshi na Jalada lake lilisomeka; MOS/RB/4669/2014 WIZI WA GARI na
kwa kushirikiana na jeshi la polisi, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa
hao wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
“Tuliwakamata wakiwa kwa mganga wa kienyeji, sikujua lengo lao kuwa
hapo ni nini, sheria itachukua mkondo wake,” alisema Alex. Kwa upande wa
Latifa alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kukamatwa mkoani
Tanga akiwa na Mose na kudai alikuwa na mpango wa kuuza gari hilo kisha
akafungue biashara.
“Wazo langu lilikuwa ni kuuza lile gari maana mume wangu alishanipa
mpaka na kadi yake, hivyo ninaamini nilikuwa nikiuza mali yangu, yule ni
rafiki yangu na sina mpango naye tena,” alisema Latifa.
Akizungumzia suala la kukamatiwa kwa Sangoma, Latifa alisema aliyeenda
ni Mose ambaye walikuwa wote na lengo lake lilikuwa ni masuala yake
ya muziki na si vinginevyo maana ni msanii.

إرسال تعليق