Mkurugenzi ahofia Tazara ‘kufa’

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Ronald Phiri amesema mamlaka hiyo inaweza kufa endapo nchi washirika hawatawekeza mtaji mkubwa ili kuongeza uzalishaji.

Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanyakazi wa shirika hilo zaidi ya 1,500 kugoma kuendelea na kazi huku wakitoa siku saba kwa uongozi wa Tazara kushughulikia madai ya mishahara ya miezi mitano.

Phiri alisema jana kuwa, hatakuwa tayari kuzungumzia kero yoyote inayotokana na migogoro ya wafanyakazi na badala yake amezitaka serikali washirika kutoa ufafanuzi wa changamoto zinazowakabili.

“Nilishatoa mapendekezo yangu muda mrefu, hivyo serikali hizo zinafahamu hatua gani zinazohitajika,” alisema Phiri.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjake alisema kwa sasa hataweza kuzungumza lolote kwa kuwa yuko likizo

Post a Comment

أحدث أقدم