MKUU
wa mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa ametaka wananchi wa mkoa wa Dodoma
kuachana na tabia yenye aibu ya kuomba chakula wakati wana fursa za
kuzalisha chakula cha kutosha, kujikimu mwaka mzima na ziada kuifanyia
biashara.
Alitoa kauli hiyo mwanzoni mwa wiki wilayani Kondoa wakati alipokuwa akizindua msimu wa kilimo mwaka 2015 kwa mkoa wa Dodoma.
Aliwataka
wananchi kutambua msimu wa kilimo, umeanza kwa hiyo wao na familia zao
wajikite kwenye kufanya kilimo ili wafanikishe azma ya kutokua ombaomba
wa chakula kila mwaka.
Katika
uzinduzi huo, ambapo pia alishiriki kwenye upandaji, Mkuu wa mkoa
alifuatana na baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Dodoma, viongozi wa
halmashauri zote za wilaya mkoa wa Dodoma na wataalamu wa kilimo kutoka
wilaya zote.
Uzinduzi
huo wa kilimo umefanyika kwa vitendo katika kijiji cha Damai Kondoa.
Gallawa alitumia nafasi hiyo pia kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri za
wilaya za Dodoma, kuhakikisha kwenye kila kijiji kunakuwa na Daftari la
Kilimo na Mifugo, ambalo litakuwa linatunza taarifa muhimu za shughuli
za kilimo na mifugo zinazofanywa na wananchi vijijini.
Akijibu
hoja ya changamoto ya soko la mazao wanayozalisha wananchi wa Dodoma,
Gallawa aliwataka wataalamu wa Serikali ya Mkoa na Wilaya wa masuala ya
biashara, kilimo, ushirika na masoko wawe wanakaa mapema kabla ya msimu
wa kilimo kuanza ili watafute masoko, ikiwezekana hata utaratibu wa
kilimo cha mkataba na kuwaelekeza wakulima mazao ya kulima kabla hata ya
msimu.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge alibainisha kuwa uzinduzi wa
Msimu wa Kilimo Kimkoa, umekuwa ukifanyika kwa miaka mitatu mfululizo
kweye wilaya za Kongwa, Chamwino na Bahi na malengo yake ni kuhamasisha
wananchi kanuni za kilimo bora.
Mshauri
wa Kilimo mkoa wa Dodoma, Bernard Abraham aliahidi yeye na wataalamu
wenziwe wa kilimo, wataendelea kubuni mikakati zaidi ya kunyanyua kilimo
mkoani Dodoma
إرسال تعليق