KAMA kawa ni Ijumaa nyingine ambayo mapaparazzi wetu, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’, Musa Mateja ‘Toz’, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ Mzee wa Mji Kasoro Bahari walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana moja kwa moja na mkuu wao aliyekuwa makao makuu za ofisi ya gazeti hili zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkuu anachjeki saa yake na kumwambia kwamban tayari ilikuwa imetimia saa nne usiku, hivyo anachukua simu yake na kuwasiliana na vijana wake waliopo sehemu mbalimbali.
Saa
4:05 usiku
DJ 2short, Kamukulu wadatisha mashabiki
Makao Makuu: Issa Mnally Mzee wa GX 100 upo pande zipi?
Mnally: Kiongozi leo nipo ndani ya Ukumbi wa Machinga Complex.
Makao Makuu: Duuh! Kuna nini hap leo?
Mnally: Mkuu hapa leo kuna uzinduzi wa disco la nguvu.
Makao Makuu: Uzinduzi wa disco? Ni nani wanazindua?
Mnally: Mkuu ni baina ya Kamukulu na Dj 2Short na wamesema mambo haya ni ya kila Ijumaa.
Makao Makuu: ahaa safi sana kuna chochote ulichokinasa hapo?
Mnally: Ndio Mkuu nimemuona Mhariri wetu za zamani wa Gazeti la Ijumaa Kessa Mwambeleko na mkewe wapo hapa.
Makao Makuu: Duuh! Kessa na mkewe wapo hapo? Kweli leo hapo patamu.
Mnally: Ndio wapo hapa pia wanamuziki wote wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ nao wapo kunogesha uzinduzi huu.
Makao Makuu: Ok endeleeni kuchapa kazi vijana wangu.
Mnally: Sawa Mkuu tupo kazini.
Saa 4:50 Usiku
MREMBO ACHOJORESHWA KILA KITU KISA BIA TATU
Makao Makuu: Habari za muda huu?
Mateja: Safi mkuu za hapo ulipo?
Mateja: Hapa safi hofu kwako, nasikia kelele sana upo mahali gani hapo?
Mateja: Mkuu nipo Barabara ya Morogoro nilikuwa Mbezi Kwa Msuguri kumuona dada’angu ila sasa hivi nipo hapa Kimara Suka Ngassa Pub.
Makao Makuu: Kuna nini hapo Ngassa Pub?
Mateja: Hapa nimepita baada ya kuambiwa kulikuwa na msanii mmoja sijui wa kundi gani amechojoleshwa nguo zote na masela na kwa bahati nzuri akajikuta akiokolewa na Mkurugenzi wa hii Ngassa Pub.
Makao Makuu: Huyo msanii alikuwa wa kike au wakiume?
Mateja: Ni mrembo na huwezi amini ni demu mmoja mkali sana na hapa tayari ameshaoga na kubadili nguo alizokuwa amevaa mwanzo na anakata kilaji kwa raha zake.
Makao Makuu: Sasa wakati anakabwa alikuwa amelewa au nini kilichotokea na hasa alikuwa akitokea wapi?
Mateja: Kutokana na maelezo ya huyu Mkurugenzi wa Ngassa Pub anasema hivi baada ya kuwahoji wale vijana waliyokuwa wakimchojolesha nguo, walidai kuwa alikuwa nao kwenye Bar moja hapo hapo Temboni baada ya kula bia za kutosha akachukua Bodaboda na kusepa si wakamuunganishia ndio wakamkamatia hapo na kuaza kudai chao.
Makao Makuu: Duuh, hivi hizo tabia za kumtemesha mtu bado zipo tu, maana hayo ni mambo ya kizamani sana, huyo demu hakuwa na fedha za kujinunulia kinywaji kweli au jamaa walijipendekeza akaamua kuwakomoa?
Mateja: Inavyoonekana huyu demu aliamua kuwanywea vibia vyao na kutimua zake maana baada ya kufika hapa Ngassa Pub, kaingia Toilet na kujipala nguo mpya na baadaye akaenda kwenye kibanda cha wakala wa simu na kutoa kama laki sasa anajinunulia bia na kuna jamaa yake anasema anakuja.
Makao Makuu: Kumbe kuna mtu alikuwa na ahadi ya kukutana naye hapo na ndiyo maana akawa anawakacha masele?
Mateja: Ndiyo mkuu inavyoonekana hata hizi fedha alizotoa ametumia na huyo bwana yake anayemsubiri hapa Ngassa Pub, huwezi amini alivyopendeza na anavyocheza muziki hapa utazani hajanywa hata pombe moja.
Makao Makuu: Duuh, huyo atakuwa kakubuu, mpe pole kwa yaliyomkuta.
Mateja: Haya bosi wangu.
Saa 5:47 usiku.
BAA YA KAMBARAGE YAZINDULIWA
Makao Makuu: Niambie wewe Mkude Simba, unasomeka pande zipi sasa?
Shekidele: Mkuu, nipo hapa katika baa iitwayo Kambarage ambayo inafunguliwa usiku huu maeneo ya Itigi.
Makao Makuu: Niambie kuna kitu gani kinaendelea hapo.
Shekidele: Watu ni wengi sana maeneo haya, pia akiwepo Polisi Kamishina, Thobias Andengenye, kama kawa naye yupo ndani ya nyumba akicheki uzinduzi huu.
Makao Makuu: Kuna mastaa wowote hapo?
Shekidele: Kama kwaida mkuu, kuna mastaa kadhaa wa sehemu hii, watu wanakunywa na kulewa, si unajua kiingilio bure.
Makao Makuu: Kumbe kiingilio bure! Kuna bendi yoyote hapo inayotumbuiza? Au uzinduzi unakwenda kimyakimya?
Shekidele: Si unajua Muumini Mwinjuma amejikita pande hizi kwa sana, sasa leo yupo na bendi yake hapa, basi ni full shangwe mkuu.
Makao Makuu: Na vipi kuhusu dada zetu, wapo?
Shekidele: Wapo mkuu tena wa kumwagwa kama wameshushwa na kontena, wapo wale wanaofanya kazi zao za kujiingizia kipato kupitia miili yao, tena hao ndiyo wametokelezea kweli, wameng’aza kinoma.
Makao Makuu: Kwa sababu muda umekwenda sana, utakapomaliza nenda kapumzike, tutawasiliana zaidi asubuhi.
Shekidele: Hakuna tatizo mkuu. Nashukuru.
إرسال تعليق