Mtoto mzuri Bongo Movies, Shamsa Ford akipozi.
MTOTO mzuri
Bongo Movies, Shamsa Ford amewabwatukia baadhi ya watu ambao wanapenda
kumsema kuwa yeye ni mshamba kwa kushindwa kutoka misele nyakati za
usiku.
Akizungumza na mwandishi wetu, Shamsa alisema anawashangaa watu hao
kumsema na kumjadili kwa watu wengine kuwa yeye ni mshamba kitu ambacho
hakipendi kwani kila mtu ana aina yake ya maisha aliyoyachagua kuishi.

Shamsa Ford (kulia) akiwa na kampani yake.
“Mimi sijawahi kumsumbua mtu hela ya kula hata siku moja kisa tu eti
sijichanganyi na wanawake wa mjini, mimi familia yangu ndiyo namba moja,
ndivyo nilivyoamua kuishi mtu akiniiita mshamba atakuwa anajisumbua
tu,” alisema Shamsa.

إرسال تعليق