Leo ni kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Cuba kwa takriban miongo
minne, Fidel Alejandro Castro Ruz maarufu kama Fidel Castro. Ni Rais
anayependwa zaidi na wanaharakati za kimapinduzi.
Moja ya vitu vinavyompa sifa katika ulimwengu huu
ni ujasiri wake wa kutoafikiana na Taifa kubwa duniani, Marekani kiasi
cha kuandamwa na kutengenezewa mitego au majaribio mbalimbali ya
kumwangamiza pasipo mafanikio.
Miongoni mwa vitu vingi ambavyo havijulikani
miongoni mwa wengi ni historia yake. Huyu jamaa alizaliwa nje ya ndoa.
Ni ‘mwanaharamu’ halisi, kama unaweza kumuita hivyo kwa lugha sanifu ya
Kiswahili.
Baba yake Castro aliyejulikana kama Angel Castro
ArgÃz alikuwa ni Mhispania aliyehamia Cuba wakati wa harakati za uhuru
wa nchi hiyo katika kipindi kati ya mwaka 1895 na 1898. Mkewe ni Maria
Luisa Argota.
Angel alikuwa ni mkulima wa miwa wa kipato cha
kati aliyeishi katika Kitongoji cha Biran, mashariki mwa nchi hiyo
pamoja na familia yake iliyokuwa na kijakazi aliyeitwa Lina Ruz
Gonzalez.
Kijakazi huyo alikuja kughilibiwa na Angel kuwa na uhusiano wa kimapenzi na ndiyo uliyosababisha kuzaliwa kwa Castro.
Katika muda wote wa ndoa ya Angel na Maria
hawakufanikiwa kupata mtoto mpaka Agosti 13, 1926 baba huyo alipompa
ujauzito binti huyo wa kazi za ndani (housegirl).
Baada ya kuzaliwa kwa Castro, Angel alilazimika
kuivunja ndoa yake na Maria na kuamua kuishi na Lina ambaye alizaa nae
watoto watano.
Castro alionekana kuwa na akili nyingi huku
akiwika katika michezo hasa ule wa magongo. Kutokana na uelewa wa haraka
aliokuwa nao tangu akiwa shule ya msingi, alisomea sheria katika Chuo
Kikuu cha Havana.
Akiwa hapo alivutiwa na siasa hivyo kujiunga na chama cha Orthodox, kilichokuwa kinapinga masuala ya ufisadi serikalini.
Mara tu alipohitimu, mwaka 1950 alifanyakazi ya uwakili akivutiwa zaidi za kesi za kisiasa.
Kutokana na mapenzi yake katika siasa, alikuwa ni mgombea wa ubunge katika Uchaguzi Mkuu uliotarajiwa kufanyika Juni, 1952.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment