Mdada huyo ambaye ameshajitwalia tuzo kadha za Oscar ndiye aliyeiongoza sinema hiyo ambayo inamzungumzia Louis Zamperini,shujaa wa vita kuu ya pili ya dunia.
Filamu hiyo ya Angelina Jolie ilioneshwa kwa wakazi wa Vatican. Lakini mkazi namba moja, Papa Francis hakuweza kuiona.
Imeelezwa kuwa papa alikutana na Angelina Jolie kwa faragha kwenye kasiri la kitume mume wa Jolie, Brad Pitt hakuwepo.
Jolie alisema kupewa nafasi ya kuonesha filamu hiyo Vatican ni heshima tosha na inaonesha kwamba Louiewa kupigiwa mfano katika masuala ya kusamehe.
Mkutano wake na Papa umefanyika miezi miwili baada ya kukaribishwa na malkia wa Uingereza,Elizabeth II kupewa tuzo ya heshima ya Order of St Michael and St George .
Amepewa heshima hiyo kutokana na juhudi zake za kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia na mchango wake katika siasa za nje za Uingereza.
Mwisho


Post a Comment