Mtoto wa Jackie Chan atupwa jela miezi 6 kwa mihadarati

Muigizaji Jaycee Chan, mtoto wa muigizaji mkali wa sinema za kung fu na komedi Jackie Chan, ametupwa jela kwa miezi sita kwa mihadarati.
Chan, 32, alikiri mbele ya mahakama kusaidia wengine kutumia mihadarati.
Polisi walivamia nyumba yake Agosti mwaka jana na kukuta gramu 100 za bangi.
Hukumu hiyo imetolewa na mahakama ya Beijing ya Dongcheng .

Mtu na baba yake

Kukamatwa kwake kumefanyika wakati wa kampeni kali ya China ya kukabiliana na ongezeko la matumizi ya mihadarati, bila kujali umaarufu wa mtu.
Chan pia alilipa faini ya Yuan 2,000 yuan ( sawa na dola322).
Jackie Chan, ambaye mwaka 2009 alitangazwa na Polisi wa china kama balozi wake wa kukabiliana na mihadarati alisema anajisikia soni kwa tabia ya mtoto wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post