Mume ambonda mke vibaya kwa kumsalimia mchungaji

hali ya mwanamke na jamaa pembeni

MWANAUME  mmoja nchini Nigeria ametembeza mkong’oto kwa mke wake wa ndoa kwa kumi na mitano kisa amezungumza na mchungaji.
Kumdunda huko kunatokana na kauli aliyompa ambayo ilimkataza mwanamke huyo kuzngumza na mchungaji huyo katika kile kinachoonekana faulo Fulani inayofanywa na mumewe itajulikana.
Mwanamke huyo anadai kwamba mumewe anatoka na mke wa mchungaji ambaye alikuwa ni rafiki yake mdada.
Mwanamama huyo ambaye anajulikana kwa jina la Comfort Oluwaseun Adebowale, ameolewa na mtu ambaye alimsaidia kumpeleka shule baada ya wazazi wake kufariki na ndugu zake kumwacha awe chokoraa.
Mwanamke huyo alisema alipomsaidia mwanaume huyo Olorode Abimbola Gbenga ambaye kwa sasa kapata kazi ya ualimu jimbo la Abeokuta Ogun  alifanya hivyo kwa mapenzi kwa kuwa alikuwa ndiye chaguo lake, alipenda kuishi naye daima.
Comfort alimsaidia mwanaume huyo mwaka 1999 akimlipia kila kitu shuleni.
“ Nilifanya hivi kwa kuamini kwamba nawekeza kwa mwanaume ambaye atakuja kuwa mume wangu, nilimpenda na nilitamani kuwa naye daima”
Lakini mambo yalianza kubadilika mwaka 2008 wakati mwanaume huyo alipopata kazi, kwani tabia yake ilibadilika, akawa anachelewa kurejea nyumbani, akawa anajibu simu kutoka kwa wanawake wasiojulikana, akawa tofauti na mbaya zaidi akaanza kumpiga.
Kwa muda wote akawa anasali akimlilia Mungu aguse moyo wake ili aweze kubadilika na kumrejesha nyumbani  lakini kila kukicha afadhali ya jana.
Mume wake kwa miaka 15 akaanza kujimwaga na rafiki wa mke wake, mtume na mke wa mchungaji katika kanisa wanalosali la Kondoo wateuliwa wa Kristo na kanisa la miujiza (shepherd of  Christ Anointed & Miracle Church), Aregbesola Eleweran Abeokuta.
Katika mazungumzo ya simu na mwandishi wa habari, mwanamke huyo aliyepigwa vibaya alisema kwamba  mumewe na mwanake huyo walianza uhusiano wa kimapenzi mwaka jana na katika hali ya kuogopa kwamba atawashika alimwelekeza kwamba hana ruksa ya kumsalimia mchungaji wao Samuel Adeniji wala kumuona akizungumza naye.
Pamoja na maagizo hayo januari 3 mwaka huu akiwa anaenda sokoni alimuona mchungaji huyo akiwa katika mlango wa kanisa lao alisimama na kumsalimia na wakati akifanya hivyo mumewe akajitokeza na kumtandika makofi palepale na kama haikutosha akanyanyua jiwe na kutandika nalo usoni huku akimwagia maneno (matusi) ambayo hayafai kunadikika huku akimlaani afe.
Comfort aliachwa kwenye dimbwi la damu na kuja kuokolewa na  wasamaria ambao walimkimbiza hospitali kwa matibabu.
Mwanamke huyo amesema kwamba amelifikisha shauri hilo Polisi, lakini  mume wake anatumia ngao ya baba mkwe ambaye alikuwa Kamishina Msaidizi wa Polisi Olorode Timothy  ambaye amestaafu ili polisi wasimsikilize wala kuchunguza suala hilo.
Oluwaseun Comfort Adebowale  amewataka wanawake  wanaopata kadhai kama yake wahakikishe wanajinasua kabla mambo hayakuwa mabaya kama yalivyo kwake.
Oluwaseun Comfort Adebowale amesema kwa wanaotaka kumsaidia anaptikana katika namba 08122174991 .
Mwandishi wa habari hii ni Mwanasheria Chukwudi Iwuchukwu ambaye yuko kwenye twita akitwiti @Chukwudi1985
mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post