Zogo la wanaume Ujerumani kujisaidia haja ndogo wakiwa wamesimama latinga mahakamani

MAHAKAMA moja  nchini ujerumani imesema wanaume wanaruhusiwa kujisaidia haja ndogo wakiwa wamesimama.
Hukumu hiyo inatokana na mwenye nyumba mmoja kumshtaki mpangaji wake akimdai fedha kibao kwa sababu ya kuharibika kwa sakafu ya chooni kunakotokana na ukung'utaji wa mkojo.
Mwenye nyumba huyo alikuwa anamtaka jamaa kulipa euro 1,900 sawa na paundi stering  za Uingereza 1400 au dola 2,200 kutokana na uharibifu uliofanyika kwenye sakafu ya choo wakati akikojoa .
Hata hivyo jaji wa Duesseldorf amesema kwamba mpangaji huyo hajakosea kukojoa akiwa amesimama kwa sababu ni sehemu ya utamaduni wa kawaida mwanaume hujisaidia kwa kusimama.
Kuna mjadala mkali nchini ujerumani kama wanaume wajisaidie haja ndogo wakiwa wamesimama au wawe wamechuchumaa au kuketi katika masinki kama wanavyofanya wanawake.
Baadhi ya vyoo vimewekewa alama ya kuzuia kujisaidia ukiwa umesimama lakini hao wanaojisaidia wakiwa wameketi wanajulikaa kijerumani kama "Sitzpinkler",ikimaananisha kwamba hawana tabia za wanaume.
Jaji Stefan Hank pamoja na hukumu yake amekubaliana  na wataalamu kwamba  mkojo unatindikali inayoweza kusababisha sakafu ya bafuni au chooni kuharibika.
Lakini alihitimisha kwamba  wanaume wanaotaka kukojoa wakisimama wajue watakuwa kidogo wanapata msukosuko kutoka kwa watu wanaoishi nao hasa wanawake lakini hawawezi kuwajibishwa kwa uharibifu unaotokea.

Post a Comment

Previous Post Next Post