Makubwa!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni
na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa
mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha
mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto.
Ilielezwa kwamba wanandoa hao walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume (jina kapuni) ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 2.
Baada ya mama mkwe kuona ishu hiyo alimwambia mwanaye Idd ambapo kwa pamoja walimpigia Saddy aliyekiri kuwa anachojua mtoto huyo ni wake na amekuwa akituma fedha za matumizi.
Mama mkwe alisema kwamba walimwita Bahati na kumuuliza kama anamfahamu Saddy ambapo alikiri kuchepuka.
Mwanamke, Bahati Ramadhani akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Baada ya mzozo wa hapa na pale, mawifi wa Bahati waliingilia kati na
kuibua bonge la mtiti wakimpa wifi yao kipigo hadi mwandishi wetu
alipotonywa na kufika eneo la tukio.Alipofika mahali hapo na kuona hali ya hatari ndipo akaita polisi wa doria ambao walifika na kutuliza ghasia.
Familia hiyo ilishuhudiwa ikiwa kwenye kikao ambapo uamuzi wa awali ulikuwa ni ldd kumuacha mara moja Bahati.
Kabla ya mambo kuwa mabaya, polisi wakiongozwa na Afande Mwajabu waliingilia kati na kumuokoa Bahati.
Afande Mwajabu aliwahoji wahusika na baada
ya maelezo, ldd alitoa uthibitisho wa kadi ya kliniki ambayo ilionesha
yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.
“Mtoto ni wangu. Kwa sasa ana umri wa miaka 2 na kadi ya kliniki ninayo.”
Saddy alipoulizwa na mwandishi wetu kwa kipindi chote cha miaka miwili, mtoto wake alikuwa akiishi wapi alisema:
Mwanamke aliyegonganisha wanaume akichepuka akichukuliwa na mapolisi kutoka eneo la tukio.
“Nilikuwa bize na masomo lakini najua mwanangu yuko na mama yake.”Kwa upande wake, Idd ambaye ndiye anayeishi na Bahati (huku akitokwa machozi) alisema hakutarajia kama mkewe angemsaliti kiasi hicho.
Bahati alipohojiwa, alisema kuwa siku aliyopata ujauzito alitembea na Saddy pamoja na mumewe ldd hivyo hata yeye anashindwa kujua baba halali wa mtoto wake.
Sakata hilo lilifikishwa polisi ambapo bado linatafutiwa suluhu.
إرسال تعليق