MKAZI wa mtaa wa Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga Regina Shija (55) ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga kichwani na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi.
Afisa
mtendaji wa Mtaa huo, Bw. Rafael Jumanne amesema kuwa tukio
hilo limetokea juzi majira ya saa 5.00 usiku ambao watu wasiofahamika
walivamia nyumbani kwa Regina akiwa anajiandaa kulala na wajukuu wake
wawili.
Amesema baada ya watu hao ambao idadi yao haijafahamika, kuvamia nyumbani hapo walianza kumkatakata mapanga mama huyo kichwani na mkono wa kulia hali iliyosababisha kuvuja damu kwa wingi baadaye kufariki dunia.
Afisa Mtendaji huyo amedai kuwa chanzo cha mauji hayo bado haijafahamika ingawa yanahusishwa na wivu wa kimapenzi na kwamba jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu huyo na kuupeleka kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na kuwa jeshi hilo linaendelea na upelelezi huku akiwaomba wananchi kulisaidia kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kulisaidia kuwabaini wahusika na hatimaye kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

إرسال تعليق