Mwanamuziki wa Nigeria Caroline Sam, al maarufu kama Maheeda katika duru za muziki ambaye alishawahi kuwa kahaba kabla ya kujiingiza katika muziki anataka ukahaba uwe ruksa nchini Nigeria.
Mwanamuziki huyu ambaye anajulikana kwa kauli
zake za kiutata na kuposti picha za mapenzi katika mitandao ya jamii amesema itakuwa vyema ukahaba ukawa ruksa.
Alisema
yapo mataifa ambayo yamesaidia sana kuhalalisha ukahaba kama ilivyo Holand na
kwamba Nigeria ikiruhusu itasaidia sana.
Alisema
pamoja na kupigwa marufuku uko kila mahali na unakuwa tatizo kwa hiyo uruhusiwe
ili uwe na vigezo vyake na mamboi yanayoambatana na biashara kama leseni na
ulipaji wa kodi kwa serikali.
إرسال تعليق