Mwarobaini sukari ya magendo waja

Dodoma. Serikali imeunda kikosi kazi kinachoratibiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kujumuisha Mamlaka ya bandari na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudhibiti sukari inayoingia kwa njia za bandari zisizo rasmi.
Hayo yalisemwa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati akitoa kauli ya mawaziri kuhusiana na suala hilo.
Amesema katika kuthibiti sukari inayoingizwa nchini, serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuunda kamati maalum ya makatibu wakuu wa wizara za kisekta.
Amesema kamati hiyo iligundua sukari inayoingizwa sokoni kinyume cha sheria ina sura tatu ikiwemo sukari inayopitia nchi jirani ambayo haifikishwi kwenye nchi iliyokusudiwa na badala yake kuuzwa nchini.
Pia sura nyingine ni sukari inayoagizwa kwa matumizi ya viwandani lakini inauzwa madukani kama sukari ya kawaida na ile inayoingia nchini kupitia njia zisizo rasmi (bandari bubu).
Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo serikali imeunda kikosi hicho kwa ajili ya kusimamia udhibiti wa sukari inayopitia nchini kwenda nchi jirani

Post a Comment

Previous Post Next Post