Mwigulu, siku 30 nyingi mno

NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba jana alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa Serikali imetoa siku 30 kwa wale wote walionufaika na fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow kulipa kodi.
Naibu waziri huyo pia alikaririwa akisema angefurahi kama wahusika wote wa sakata la Escrow wangekamatwa kwa sababu kutofanya hivyo ni kama kile alichoita kuwafanyia wahalifu hafla ya kuwaaga send-off.
Naibu waziri huyo alisema kuwa ni lazima kodi ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ili zitumike katika huduma za jamii kwa wananchi na kwamba watu hao kuachwa wakidunda baada ya kuikosesha Serikali mapato yake si sahihi.
Nia njema iliyoko kwenye kauli za Mwigulu kuhusu kodi iliyokoseshwa Serikali na watu hao, hailingani na siku 30 zilizotolewa naye kwa watu hao kulipa kodi stahiki kutokana na kipato hicho cha wahusika.
Kauli ya Mwigulu aliitoa baada ya kutembelea Hospitali ya Mwananyamala na kujionea uhaba mkubwa wa vifaa kwa wagonjwa wanaolazwa au kutibiwa.
Nasi tunadhani kuwa kama kweli Mwigulu aliguswa na matatizo hayo asingetoa siku 30 kwani kwetu sisi tunaona ni nyingi mno kulingana na mahitaji ya kodi hizo kuimarisha huduma za jamii.
Uhaba wa vitanda katika Hospitali ya Mwananyamala ni mfano mdogo tu wa matatizo ya hospitali nyingi nchini.
Wajawazito wanajifungulia chini, hospitali zinakosa dawa Mwigulu analijua hilo na kutoa siku 30 ni kuonesha kuwa hajaguswa na matatizo wanayopata wananchi na badala yake anawaachia watu haowaendeleekuneemekana fedha hizo.
Sisi tunaamini kuwa hii si haki na ni dhambi kubwa mno kuendelea kuwaachia waliokwisha neeme kakuendelea kuneemeka kwa gharama ya watu wa kima cha chini.
Tunajiuliza kwa nini watu hao wanaotuhumiwa kuingiziwa fedha za Escrow hawakulipa kodi tangu wakati huo walipozichota fedha hizo?
Kama isingekuwa Kamati ya Zitto maana yake serikali ingekosa fedha zote hizo? Mbaya zaidi kwa nini tena serikali itoe siku 30 badala ya kusema mara moja?
Inashangaza kwani itakumbukwa kuwa sakata la Escrow liliibuliwa miezi mingi iliyopitana ni dhahiri kuwa waliingiziwa kwenye akaunti zao mwanzoni mwa mwaka jana na sasa Mwigulu anatoa maagizo walipe kodi.
Hili ni agizo la pili kwa kiongozi huyo, kwani Desemba mwaka jana alitoa agizo kama hilo lakini hadi leo bado halijatekelezwa na cha kushangaza zaidi badala ya kuchukua hatua anawapa tena siku 30, kama walishindwa kutekeleza katika agizo la kwanza kuna uhakika gani kama agizo la pili litatekelezwa?
Tunajiuliza kama kweli ipo nia ya dhati ya kuwatendea haki wananchi, siku 30 ni nyingi na kimsingi angeweka muda mfupi zaidi ili wahusika walipe  kodi husika haraka na hatimaye ziende kwenye maendeleo.

Post a Comment

Previous Post Next Post