Kupanga bei ya bidhaa au huduma ni mchakato unaohusisha vitu
vingi. Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya biashara wanasema kuwa kuna
njia kuu nne zinazotumika katika upangaji bei ya bidhaa au huduma. Njia
hizo ni; kwanza kupanga bei kwa kuzingatia gharama za uzalishaji wa
bidhaa husika. Kimsingi, mjasiriamali anayetumia njia hii anatakiwa
kupanga bei kwa kutumia mbinu zifuatazo:
Yaani, wajasiriamali wanaonunua bidhaa kwa ajili
ya kuuza. Kwa mfano, kama bei ya kitabu kulingana na bei ya mchapishaji
ni Sh15,000 muuzaji anaweza kuongeza kiasi cha shilingi 2,000 katika bei
ya mchapishaji na hivyo kuwa Sh17,000.
Kadhalika, njia hii hupendwa sana kutumiwa na wajasiriamali ambao hawazalishi bidhaa kwani huwapatia kile wanachokitaka.
Pili ni njia ya gharama za uzalishaji, ambayo
hutumiwa sana na wazalishaji wa bidhaa. Mzalishaji wa bidhaa hukadiria
gharama za kila bidhaa moja pamoja na gharama za kawaida za uzalishaji
na uuzaji wa bidhaa husika. Faida huongezwa katika gharama za uzalishaji
wa kila bidhaa moja.
Tatu ni gharama na mahitaji ya bidhaa, ambayo
hujumuisha gharama za moja kwa moja zinazotokana na uzalishaji wa bidhaa
husika. Njia hii hutumiwa zaidi mahali ambapo kuna soko la ushindani
ambapo bei hutumika kama njia moja ya kukamata soko.
Nne ni upangaji bei wenye kukwepa hasara ambayo
hutumiwa ili kuhakikisha kuwa matumizi/gharama na mapato ya biashara
huwa na uwiano sawa. Matokeo yake huwa ni kutokuwa na faida wala hasara.
Hata hivyo, pale ambapo hutokea mapato yakazidi matumizi, faida
hupatikana na kinyume chake ni hasara. Makampuni mengi hutumia njia hii
kwa lengo la kufikia hatua fulani walojiwekea katika uzalishaji au
hutoaji huduma itakayowapekea kupata faida.
Tano ni upangaji bei kwa kuzingatia mahitaji kwani
baadhi ya wajasiriamali wanaamini kuwa uwezo wa wateja wao katika
kununua bidhaa zao huwawezesha kupata faida wanayoitegemea.
Wajasiriamali wanaotumia njia hii uzingatia mbinu za uenguaji, ambapo
mjasirimali anaweza kuuza bidhaa zake kwa bei ya juu kwa lengo la
kuhudumia watu wa aina fulani tu.
Vilevile, hutumia mbinu ya upenyaji kwa lengo la
kutaka kupenya katika soko fulani na kuwa mdau wa soko husika. Pia
hutumia mbinu ya kutoza kile mteja anaweza kumudu kwa kuzingatia gharama
za huduma na thamani ya huduma.
Sita ni upangaji bei kwa kuzingatia ushindani
uliopo, ambapo mjasiriamali anapojua barabara wanachofanya washindani
wake anakuwa katika nafasi nzuri ya kupanga bei ambayo italeta ushindani
kwa lengo la kumnufaisha. Njia hii hutumia mbinu zifuatazo katika
kupanga bei; punguzo la bei, ambapo mjasiriamali hutoa punguzo la
asilimia fulani kwa kila bidhaa moja kutoka katika bei halisi. Mbinu hii
hutumiwa kwa ajili ya kuwavutia wanaonunua bidhaa kwa ajili ya kuziuza
tena.
Vilevile, hutumia mbinu ya kuuza bidhaa/huduma kwa
bei kubwa kwa lengo la kuhudumia watu wenye kipato cha juu peke yake.
Mbinu hii hutumiwa na makampuni, ambayo hayaoni umuhimu wa kuhudumia
kila mtu. Kwa maneno mengine, ni mbinu ambayo hutumiwa kwa ajili ya
kukusanya kikubwa.
Post a Comment