Namna ya kupanga bei za bidha au huduma

Kupanga bei ya bidhaa au huduma ni mchakato unaohusisha vitu vingi. Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya biashara wanasema kuwa kuna njia kuu nne zinazotumika katika upangaji bei ya bidhaa au huduma. Njia hizo ni; kwanza kupanga bei kwa kuzingatia gharama za uzalishaji wa bidhaa husika. Kimsingi, mjasiriamali anayetumia njia hii anatakiwa kupanga bei kwa kutumia mbinu zifuatazo:
Yaani, wajasiriamali wanaonunua bidhaa kwa ajili ya kuuza. Kwa mfano, kama bei ya kitabu kulingana na bei ya mchapishaji ni Sh15,000 muuzaji anaweza kuongeza kiasi cha shilingi 2,000 katika bei ya mchapishaji na hivyo kuwa Sh17,000.
Kadhalika, njia hii hupendwa sana kutumiwa na wajasiriamali ambao hawazalishi bidhaa kwani huwapatia kile wanachokitaka.
Pili ni njia ya gharama za uzalishaji, ambayo hutumiwa sana na wazalishaji wa bidhaa. Mzalishaji wa bidhaa hukadiria gharama za kila bidhaa moja pamoja na gharama za kawaida za uzalishaji na uuzaji wa bidhaa husika. Faida huongezwa katika gharama za uzalishaji wa kila bidhaa moja.
Tatu ni gharama na mahitaji ya bidhaa, ambayo hujumuisha gharama za moja kwa moja zinazotokana na uzalishaji wa bidhaa husika. Njia hii hutumiwa zaidi mahali ambapo kuna soko la ushindani ambapo bei hutumika kama njia moja ya kukamata soko.
Nne ni upangaji bei wenye kukwepa hasara ambayo hutumiwa ili kuhakikisha kuwa matumizi/gharama na mapato ya biashara huwa na uwiano sawa. Matokeo yake huwa ni kutokuwa na faida wala hasara. Hata hivyo, pale ambapo hutokea mapato yakazidi matumizi, faida hupatikana na kinyume chake ni hasara. Makampuni mengi hutumia njia hii kwa lengo la kufikia hatua fulani walojiwekea katika uzalishaji au hutoaji huduma itakayowapekea kupata faida.
Tano ni upangaji bei kwa kuzingatia mahitaji kwani baadhi ya wajasiriamali wanaamini kuwa uwezo wa wateja wao katika kununua bidhaa zao huwawezesha kupata faida wanayoitegemea. Wajasiriamali wanaotumia njia hii uzingatia mbinu za uenguaji, ambapo mjasirimali anaweza kuuza bidhaa zake kwa bei ya juu kwa lengo la kuhudumia watu wa aina fulani tu.
Vilevile, hutumia mbinu ya upenyaji kwa lengo la kutaka kupenya katika soko fulani na kuwa mdau wa soko husika. Pia hutumia mbinu ya kutoza kile mteja anaweza kumudu kwa kuzingatia gharama za huduma na thamani ya huduma.
Sita ni upangaji bei kwa kuzingatia ushindani uliopo, ambapo mjasiriamali anapojua barabara wanachofanya washindani wake anakuwa katika nafasi nzuri ya kupanga bei ambayo italeta ushindani kwa lengo la kumnufaisha. Njia hii hutumia mbinu zifuatazo katika kupanga bei; punguzo la bei, ambapo mjasiriamali hutoa punguzo la asilimia fulani kwa kila bidhaa moja kutoka katika bei halisi. Mbinu hii hutumiwa kwa ajili ya kuwavutia wanaonunua bidhaa kwa ajili ya kuziuza tena.
Vilevile, hutumia mbinu ya kuuza bidhaa/huduma kwa bei kubwa kwa lengo la kuhudumia watu wenye kipato cha juu peke yake. Mbinu hii hutumiwa na makampuni, ambayo hayaoni umuhimu wa kuhudumia kila mtu. Kwa maneno mengine, ni mbinu ambayo hutumiwa kwa ajili ya kukusanya kikubwa.

Post a Comment

أحدث أقدم