Zanzibar. Wakati Kamati Kuu ya CCM, ikieleza
kusikitishwa kwake na baadhi ya viongozi wake walio katika dhamana ya
kisiasa kukumbwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow, adhabu kali
zitachukuliwa dhidi ya wagombea urais sita walioadhibiwa mwaka jana
endapo walikiuka masharti ya adhabu zao.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alisema jana baada ya Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana Ofisi Ndogo ya
CCM, Kisiwandui kuwa kamati hiyo imeagiza Kamati Ndogo ya Maadili
kushauri na kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi watakaokuwa
wamekiuka adhabu husika.
“Itakumbukwa kuwa kuna makada sita wa CCM
waliopewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato
wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao
Februari mwaka huu.
“Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika
tathimini kuona kama walizingatia masharti ya adhabu zao na kama kuna
ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao, wataongezewa
adhabu,” alisema Nape.
Vigogo sita waliopewa adhabu ni; Waziri Mkuu
Mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira .
Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Nape alisema kamati ndogo ya maadili inayoongozwa
na makamu mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula itatoa ushauri kwa
ngazi za juu za CCM na ikibidi hatua nyingine za kinidhamu na kiatiba
zitafuata.
Makamba asema
“Binafsi sina wasiwasi, kwanza mwanzoni sikustahili kuwemo na hata sasa sina shaka kama kuna lolote nililofanya kinyume.”
Alisema kuwa wanaopaswa kuwa na wasiwasi ni wale
wanaogawa pesa. “Sisi wengine hizo fedha hatuna...ninaamini wapo wengine
ambao hawapo kwenye orodha lakini wamekiuka maadili. Nilitarajia na wao
watahojiwa,” alisema Makamba.
Sumaye akumbushia rufani
Akizungumzia hatua hiyo ya Kamati Kuu, Sumaye
alisema: “Mimi siwezi kujitathmini mwenyewe, tusubiri hiyo kamati tuone,
sijui watasema nini na wala sielewi kosa langu na ndfiyo maana nilikata
rufani- Mwananchi
إرسال تعليق