RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju
kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana,
Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5,
2015, Ikulu, Dar Es Salaam. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa
Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
NEWS: RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA MWANASHERIA MPYA KUCHUKUA NAFASI YA WEREMA
Hisia
0
Post a Comment