Kingunge Ngombale Mwilu.
Heshima yako mzee! Najua una mambo mengi ya kufanya, ukichanganya na
umri wako, itakuwa vigumu sana kwa mtu kama mimi kuonana ana kwa ana na
wewe. Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya niamue kutumia ukurasa huu
kufikisha ujumbe wangu kwako.
Mheshimiwa, mimi si mwanasiasa mkongwe kama wewe ambaye umeitumikia
nchi hii tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka leo hii.
Sijawahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye nchi hii, zikiwemo ukuu wa
mikoa kadhaa, ubunge wala uwaziri. Wala sijawahi kuwa mwanaharakati wa
kusimamia ujamaa kama wewe.
Sijui chochote kuhusu siasa, utawala wala historia ya nchi hii,
niponipo tu, kama bendera inayofuata upepo. Hata hivyo, ningekuwa mimi
kwenye nafasi yako, nakuhakikishia mzee nisingefumbua mdomo wangu
kuwananga wote waliojitokeza kuwania urais kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM) bila kwanza kujifanyia tathmini mimi mwenyewe juu ya uadilifu
wangu.
Kila mtu anao uhuru wa kuzungumza mawazo yake hadharani, naamini na
wewe uliitumia vyema haki yako hiyo ya kikatiba, hivi karibuni
ulipoonekana na kusikika kupitia kituo kimoja cha runinga ukisema wote
waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha
kutaka kuingia ikulu.
Sipingi ulichokisema, ni kweli kwa kipindi kirefu imekuwa ni kawaida ya wanasiasa au watawala waliopo madarakani, kutumia fedha kama njia ya mkato ya kuwafanya wapate nafasi za juu za uongozi, hilo liko wazi na hakuna asiyelijua.
Sipingi ulichokisema, ni kweli kwa kipindi kirefu imekuwa ni kawaida ya wanasiasa au watawala waliopo madarakani, kutumia fedha kama njia ya mkato ya kuwafanya wapate nafasi za juu za uongozi, hilo liko wazi na hakuna asiyelijua.
Kinachonishangaza, kwa nini kauli yako hiyo ije leo? Mheshimiwa,
umekuwa kwenye siasa kwa kipindi kirefu sana, umeona mengi na naamini
hata hili ulilolisema hivi karibuni, ulikuwa ukilijua kwa kipindi kirefu
na kwa namna moja au nyingine ulikuwa ukiliunga mkono ndiyo maana licha
ya kushika nyadhifa nyingi kubwa kwenye taifa hili, hujawahi kuisaidia
serikali kupambana na viongozi wa aina hiyo.
Kama nimesahau nikumbushe mzee, ni lini ulipoisaidia au kuishauri
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) au jeshi la polisi
kuwanasa watu wa aina hiyo? Kama hujawahi kufanya hivyo wakati ulikuwa
unajua faulo zilizokuwa zikichezeka kwa kipindi kirefu, basi na wewe ni
miongoni mwa wacheza faulo.
Ndiyo! Licha ya mchango wako mkubwa katika siasa za nchi hii,
misimamo yako inatia shaka mzee. Kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,
Kanisa Katoliki Tanzania lilitoa waraka wa kuwaelekeza waumini wake kuwa
makini na wanasiasa waliokuwa wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi na
kuwataka kutowapa nafasi viongozi wanaoendekeza rushwa na kusahau
matatizo ya wananchi.
Mzee, wewe ulikuwa miongoni mwa watu walioupinga vikali waraka huo,
ukaingia kwenye malumbano makubwa na viongozi wa kidini, umesahau?
Kwamba kitendo cha kanisa kuwatahadharisha waumini wake kutowachagua
wala rushwa kilikukera sana. Leo na wewe unazungumza kitu kilekile, kipi
kilichokufanya ubadilike na kuwa na misimamo isiyoeleweka?
Watanzania bado hawajasahau jinsi familia yako ilivyohusishwa na
kampuni ya kukusanya ushuru kwenye Stendi ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya
Ubungo (Ubungo Bus Terminal), iliyoisababishia serikali upotevu wa
mabilioni ya shilingi.
Historia yako inakuhukumu mzee, ingekuwa vyema kama ungejitathmini
kwanza kabla ya kutoa kauli hiyo kwa sababu inawafanya wengi washindwe
kukutafsiri unasimamia upande gani.
Wasalaam.
Wasalaam.
إرسال تعليق