Kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
Na Mwandishi Wetu
SIKU moja baada ya uongozi wa Simba kutangaza kuachana na kipa Juma Kaseja, sasa unalazimika kupambana na kesi mpya dhidi ya kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi.
SIKU moja baada ya uongozi wa Simba kutangaza kuachana na kipa Juma Kaseja, sasa unalazimika kupambana na kesi mpya dhidi ya kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kupitia mwanasheria wake, Kampuni ya Agaba Muhairwe & Co
Advocates ya Kampala, Uganda. Okwi amefungua kesi akitaka Yanga imlipe
kitita cha jumla ya dola 62,000 (zaidi ya Sh milioni 107).
Mgawanyo wa madai hayo umegawanywa mara mbili, ukianza na dola 50,000 ambazo Okwi anaidai Yanga aliposajili ikiwa alilipwa nusu yake.
Mgawanyo wa madai hayo umegawanywa mara mbili, ukianza na dola 50,000 ambazo Okwi anaidai Yanga aliposajili ikiwa alilipwa nusu yake.
Pili, mshahara wake, dola 12,000 ambao pia hakulipwa na Yanga. Jumla inakuwa dola 52,000.
Tayari Agaba Muhairwe & Co Advocates wamewasilisha barua yenye kumbukumbu namba AM/129/ea kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji.
Barua hiyo ya Januari 7, kopi mbili, moja imewasilishwa kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na nyingine kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Mwanasheria huyo wa Okwi amesisitiza kwamba hawatafungua kesi yoyote
kwa kuwa wanatoa hadi Februari 15 kuwa wameishalipwa fedha hizo.Sehemu
ya barua hiyo inaonyesha barua ya juzi inakumbushia barua nyingine kama
hiyo ambayo kampuni hiyo ya mwanasheria iliitoa na kutaka Okwi awe
amelipwa hadi Desemba 15, mwaka jana lakini haikufanyika.
Maana yake, iwapo Yanga watashindwa kufanya hivyo watakuwa tayari
kufungua kesi ya madai kuhakikisha wanapata fedha zao na haina ubishi
watakwenda Fifa ambayo wameisha itaarifu kuhusiana na deni hilo.
Okwi aliondoka Yanga baada ya uongozi kumtema katika hatua za mwisho
za usajili wa dirisha dogo na Simba ikamsajili, hali iliyozua tafrani
kubwa. Baadaye TFF ilimpitisha Okwi kuichezea Simba na Yanga haikuwa
imekubaliana na uamuzi huo.
Post a Comment