NI
kwa blesi za Saa God makachaa tunamiti wansi ageini katika kijiwe chetu
cha kujipa maraha, ama nini? Najua kitu cha mwezi dume, apecha alolo
ndo kinasogea kwa mbaliii. Makidi wanataka kwenda skonga, fulu kutaka
mazagazaga ya skuli nini na nini, shigidishida!
Mbaya zaidi wao hawajui kama jua limewakia mifukoni, mifuko imetoboka
chezea mbishe za Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya! Wao wanakomaa tu
ili watimize wajibu wao wa kupiga msuli. Jichangechange kama vipi mwezi
dume utapita na laifu litakaa kwenye mstari.
Tukirudi kwenye mastori yetu ya tauni, masela wa Panya Road ndiyo
habari ya mujini. Wanawafanya maraia waishi kwa fasi ya uoga fulu stresi
utadhani wako Dafuu au Iraki. Baa zote mastori ni Panya Road, vijiwe
vyote ishu ni hiyohiyo.
Enewei ngoja niwape mchapo mmoko wa mwanangu Wile. Kama unavyojua
tena mwezi dume unaendelea lakini mwana akakamata mchuchu wake wa longi
taimu, aliulia taimingi kinoma lakini siku hiyo ukaingia kingi.
Huku na huku nini na nini baada ya kumtwangia mafoni, wakamiti katika
baa moko iliyopo maeneo ya Sinza Kijiweni. Nisiwafiche wazazi, mtoto ni
mtoto kweli, ana hoja kama vile kachorwa.
Mwana akachili naye katika kona f’lani yenye kitu cha mwanga hafifu kama unavyojua tena engo za malovee zinavyohusika.
Mwana akachili naye katika kona f’lani yenye kitu cha mwanga hafifu kama unavyojua tena engo za malovee zinavyohusika.
Mdogomdogo kama songi la Diamond, jamaa akamuagizia kitu chupa kubwa
lenye kilevi. Yeye akavuta Konya kubwa akawa anamiksi na maji makubwa
huku mtoto mkaree akifyonza asteaste mvinyo wake. Muziki laini ulikuwa
ukichombezachombeza, kinywaji kikaanza kufika mahali yake, wakaagiza
manyamanyama si unajua tena pombe dawa yake kujichana? Chukua hiyo!
Stori za kuamsha hisia za malovee zikawa zinashuka pale kati, ghafla
bin vuu masela wa meza ya mbele wakaibuka na kuanza kutimua mbio, mwana
akatahamaki kutaka kujua nini kinaendelea, mubebizi ukachomoka nduki.
Mwana akasikia; “Panya Road...Panya Road...Panya Road.” Kusikia
hivyo, mwana akasepa, pale mezani akaacha pochi ya mubebizi, simu zake
za kutachi kama tatu akakimbilia toileti ya kike.
Baada ya dakika kama tano hivi, hali ikatulia na waliporudi katika meza yao wakakuta wana wamesafisha kila kitu, pamebaki peupeee!
Baada ya dakika kama tano hivi, hali ikatulia na waliporudi katika meza yao wakakuta wana wamesafisha kila kitu, pamebaki peupeee!
Mwana stimu zote za mitungi zikakata, hakuwa na hamu tena ya kuponda
raha. Alikuwa na mtonyo kwenye waleti ikabidi amsalimishe mtoto homu
kwao na yeye akatimba zake magetoni akapindua.
Kitu cha msako ndo kikaanza kusanuka kitaani. Big up kwa Afande Suleiman Kova kozi naiti ileile aliingia kitaani na kuanza kuwatilia timu makamanda wake waliokuwa wakipiga misele katika viunga mbalimbali vya jiji!
Kitu cha msako ndo kikaanza kusanuka kitaani. Big up kwa Afande Suleiman Kova kozi naiti ileile aliingia kitaani na kuanza kuwatilia timu makamanda wake waliokuwa wakipiga misele katika viunga mbalimbali vya jiji!
Kova alitisha kinomanoma baada ya kutimba kwenye Televisheni ya Taifa
TIBISII na kuwaondoa shaka wanyamwei wote kwamba wambonji kwani mamwela
kibao wapo mitaani wakipiga doria.
Olu in olu, masela kitaani tunatakiwa kujikontroo wenyewe na michongo
kaa hii ya Panya Road ni mizinguo. Washua ambao mnajua makidi wenu
wanapiga hizo mbishe ni bora mkawaonya kabla hawajaingia kwenye mikono
ya mwela wa Kova.Amani ya kitaa inaanza na mimi na wewe, kila mtu aplei
pati yake na maisha yatakuwa burudani.
Sii yuu nexti wiki mazee, mzuka mwingi!
Sii yuu nexti wiki mazee, mzuka mwingi!

إرسال تعليق