Polisi hao wamefanya mauaji hayo wakati wakijaribu kuwadhibiti watuhumiwa hao ambao walikuwa na mateka.
Polisi wamesema kwamba mateka huyo ametoka salama.
Milipuko ilisikika jioni katika kiwanda cha uchapaji wakati polisi maalumu walipovamia eneo hilo kukabiliana na watuhumiwa hao ambao walikuwa na mateka mmoja.
Aidha Polisi walivamia soko la kosher ambako marafiki wa ndugu hao wawili nako walikuwa wakishikilia idadi isiyojulikana ya mateka muda mfupi baada ya kuanza kwa kazi katika kiwanda.
Baadhi ya mateka katika sekeseke hilo walitoka salama.

إرسال تعليق