Polisi
Jijini Dar es Salaam wamelazimika kufyatua risasi hewani na kufyatua
mabomu ya machozi kufuatia kuibuka kwa vurugu katika hoteli ya Land Mark
ambapo shughuli ya uapishaji wa wenyeviti wa serikali Mitaa
zinafanyika.
Vurugu hizo, zimeibuliwa
na kambi ya upinzani ambayo imelalamikia kuwa Mwenyekiti mmoja wa Chama
tawala CCM aliyeapishwa hakuwa ameshinda katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa, uliofanyika mwaka jana.
إرسال تعليق