Roda; binti aliyelipiwa kishika uchumba akiwa na miaka 15

“Natamani kuondoka eneo hili lenye mila na desturi nyingi potofu zinazoninyima haki, sina amani hata kidogo na moyoni mwangu sioni nuru ya maisha yangu”
“Kwa mfano tarehe 11.06.2014 alikuja mwanamume mmoja nyumbani kwetu akampa mama kilo moja ya sukari na Sh500 kama kishika uchumba ili anioe katika umri huu mdogo”.
Maneno haya ya kukata tamaa yanatoka kinywaji mwa Roda Damas (jina halisi limefichwa), mwanafunzi wa Shule ya Msingi Oldonyomurwa iliyopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Roda mwenye umri wa miaka 15 ni miongoni mwa watoto wa kabila la Wamasai ambaye anatakiwa kuolewa katika umri mdogo, baada ya wazazi wake kupewa kishika uchumba na mwanamme anayenuia kumuoa.
Hofu hii ya watoto wa jamii ya kifugaji ndiyo inayonifanya nitembelee maeneo yao kuujua ukweli wa yanayozungumzwa na nina bahatika kukutana na Roda anayezungumza nami huku akibubujikwa machozi.
Wilaya ya Siha hususan Kata za Orkolili, Makiwaru, Karansi, Gararagua na Biribiri, zina watoto wa kike wanaoishi kwa hofu ya kuolewa katika umri mdogo. Wengine wanaanzia hata miaka mitano.
Ndoa za utotoni
Roda anasema kwa jamii ya kifugaji si jambo la ajabu mtoto kuchumbiwa hata akiwa na umri wa miaka mitano, umri ambao hata anayechumbiwa hajui nini kinaendelea.
“Mwanamume anaweza kuja na kutoa kishika uchumba na mtoto ataendelea kuishi kwa wazazi wake na siku akimhitaji humchukua baada ya kutoa ng’ombe waliohitajika kama mahari.
“Kila nikipita nikikutana na huyo baba huniita mke wake na hata mama yangu huniambia huyo ndiye mume wako. Hii inaniumiza kwa sababu mimi nataka kusoma sitaki kuolewa.”
Hawa nao wako mtegoni
Roda ananisaidia kukutana na watoto wengine wawili, Neema na Evelyn wote wana miaka 14 na wana masaibu kama yake kwani tayari wameonyeshwa wachumba na wanatakiwa kukeketwa ili waolewe.
Soma zaidi Hapa

Post a Comment

أحدث أقدم