Dar es Salaam. Akiwa na kaptula pana, tumbo
wazi huku amebeba beleshi, Ally Bakari ‘Champion’, bondia wa zamani wa
masumbwi na mkazi wa Mtaa wa Buguruni Kisiwani, anawaongoza wenzake
kwenda kuzibua mtaro wa maji taka ambao umeziba na kuzua mtafaruku
mtaani hapo.
Anafanya hivyo si kwa vingine isipokuwa ni
kutokana na hulka yake ya kutokupenda kuacha mambo yakiharibika wakati
uwezo wa kuyarekebisha upo.
Safari yao hiyo inafikisha eneo hilo na kwa
jitihada zao wanafanikiwa kuyazuia yasitiririke katika makazi ya watu
lakini hata hivyo bado yanamwagika.
Mkazi huyo anachukua hatua za ziada ikiwa ni
pamoja na kuwasiliana na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Taka Dar es
Salaam (Dawasa), ambao wanafika na kutatua tatizo.
Tukio hilo ni moja kati ya mengine yanayomhusisha
mkazi huyo, likiwamo la eneo linalodaiwa limeuzwa ambalo awali
lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya
Buguruni.
Jitihada zake hizo hata hivyo zinagonga mwamba
kwani kunabainika kwa kuwa walioliuza ndiyo waliyopelekewa malalamiko
hayo, kwani mwitikio hakuna.
Huyo ndiyo Championi, mwanaharakati wa maendeleo
ya kijamii ambaye ili kuweza kuona anapata nafasi ya kutekeleza dhamira
yake ya kuwatumikia wananchi kwa kuwashirikisha kutatua kero zao.
Ni mmoja wa watu waliomba nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Kisiwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF).
Hata hivyo, anachokiona wakati wa kupiga kura
kutafuta mgombea wa nafasi hiyo ndani ya chama, kinamfanya afikirie mara
mbili kuhusiana na dhamira za wanasiasa kwa wananchi wanapowania nafasi
mbalimbali za uongozi.
Anasema yeye ndiye aliyekuwa chaguo la wakazi wa
Kisiwani kwa mapenzi yao toka moyoni na siyo kwa vishawishi vya pesa au
vitu vingine vya namna hiyo.
Anabainisha kuwa siku ya upigaji wa kura mambo
mengi ya ajabu yalijitokeza kwani licha ya kuongoza muda mrefu huku kila
mmoja akijua kuwa yeye ndio chaguo la chama hicho, anasema alishangaa
kuona wapiga kura hawaishi na mbaya zaidi vikao visivyo rasmi nje ya
ukumbi.
“Wanachama waliandika barua, ofisi ya kata, wilaya
hadi mkurugenzi wa Taifa wa uchaguzi anatambua hilo lakini hakuna hatua
za maana ziliozochukuliwa,” anasema na kudai kuwa:
Post a Comment