Jana katika gazeti hili tulichapisha habari iliyokuwa ikieleza
kuwa Polisi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),
inamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na kenge 149, kati yao
134 wakiwa hai akidaiwa kutaka kuwasafirisha.
Habari hiyo ilimkariri Kamanda wa Polisi wa JNIA,
Khamis Suleiman akimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed Ally
Mansour (34) na kwamba alikamatwa juzi saa tano usiku alipokuwa
akijiandaa kwenda Kuwait kupitia Dubai kwa Shirika la Ndege la Emirates.
Mansour alikamatwa na kenge hao akiwa amewahifadhi kwenye mifuko midogomidogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.
Wakati wanamfanyia upekuzi, maofisa usalama ndipo
walipogundua kuna vitu ambavyo vinafanana na nyoka na kuamua
kuwashirikisha wataalamu wa maliasili ambao walibaini kuwa ni viumbe
aina ya kenge. Tunachukua nafasi hii kuipongeza Polisi kwa kitendo cha
kukamatwa kwa raia huyo wa Kuwait akiwa na kenge hao.
Hata hivyo, tunaamini kuwa kukamatwa kwa raia huyo
akiwa na wanyama hao uwanja wa ndege, ni ishara kwamba kuna watu wengi
wanasafirisha wanyama wetu kwenda nje ya nchi kinyemela.
Ni jambo la kushangaza kuona kwamba pamoja na
Serikali kuapa kwamba kwa sasa imedhibiti mianya ya utoroshaji wa
wanyama hai kinyemela kwenda nje ya nchi, lakini ukweli ni kwamba
wanyama hao bado wanatoroshwa.
Tunajuliza, kama huyu raia wa Kuwait amediriki
kujaribu kupitisha kenge hao uwanja wa ndege, je, wanyama wangapi
watakuwa wanasafirishwa kupitia njia za panya katika maeneo mbalimbali?
Ni wazi kuwa ni wengi.
Ni wazi kuwa raia wa Kuwait atakuwa na mtandao
hapa nchini, haiwezekani amekuja Jumanne halafu siku ya inayofuata
anasafiri kwenda nchini kwao akiwa na kenge tena wapatao 149.
Hili siyo tukio la kwanza kwa wanyama kukamatwa
wakisafirishwa kinyemela kwenda nje ya nchi. Inavyoonyesha pamoja na
kuwapo kwa matukio hayo, bado hatujajifunza kama vile wanaotoroshwa siyo
mali yetu ya asili.
Mwaka 2013 shehena kubwa ya meno ya tembo ikiwa na
vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini
ilinaswa katika Bandari ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa
serikali zote mbili wakiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii wakati
huo, Khamis Kagasheki.
Shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa
kuelekea Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na
magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya
baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena.
Kama hiyo haitoshi mwaka huohuo, meno 706 ya ndovu yalikamatwa jijini Dar es Salaam

إرسال تعليق