Kikosi cha Simba sc kilichoanza
WEKUNDU
wa Msimbazi wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la
Mapinduzi kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vinara wa ligi
ya Zanzibar, JKU katika mechi iliyomalizika usiku huu uwanja wa Amaan
Zanzibar.Bao
pekee la Simba limefungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ katika dakika ya
11 kwa shuti kali akipokea pasi murua ya Said Ndemla.
![SAM_4332](http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/SAM_4332.jpg)
Kikosi cha JKU kilichoanza
Kwa
matokeo hayo, Simba wameibuka vinara wa kundi C kwa kujikusanyia pointi
6 kibindoni, huku nafasi ya pili ikishikwa na Mtibwa Sugar wenye pointi
tanoSimba walianza mchezo kwa kasi, lakini JKU walionekana kuchakarika kuwadhibiti wakali hao wa Msimbazi.Kikosi
cha Mnyama kinachonolewa na Mserbia Goran Kopunovic kimeonekana kucheza
mpira wa kasi na pasi za uhakika kuanzia sehemu ya ulinzi na safu ya
ulinzi.Baada ya mechi hiyo, kocha Kopunovic amesema timu yake inaimarika kidogo kidogo na ilicheza tofauti kwa vipindi vyote.
“Hii ni siku ya tano tu tangu nifike, bado naendelea kuwapa mbinu mpya. Wachezaji wangu kimbinu nawaona wazuri”
“Mimi napenda vijana ndio maana nawatumia wengi. Kidogo kidogo tutakuwa safi” Alisema Kopunovic.
Simba wanasubiri mpinzani wao wa Robo fainali katika mechi za kesho ambapo kutakuwa na mechi nne.
Majira
ya saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Amaan, KCC watachuana na KMKM, saa
11:00 jioni Azam fc watakabiliana na Mtende, hizo ni mechi za kundi B.
Kundi A, Taifa ya Jang’ombe itapepetana na Polisi katika uwanja wa Mao Dze Tung majira ya saa 9:00 alasiri.
Mtanange mwingine wa kundi A utawakutanisha Yanga dhidi ya Shaba majira ya saa 2:00 usiku uwanja wa Amaan.
إرسال تعليق