Leo
tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika
familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao
za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa
kupata watoto.
Kuna wengine wanapata watoto au mtoto mmoja na baadaye wanashindwa
kupata mtoto kwa sababu ya mimba zao kuwa zinaharibika mara kwa mara.
Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba asilimia 50 ya mimba zote huwa
zinaharibika, najua watu wengi wanaweza wakashangaa lakini ni kweli
tafiti za kitabibu zinasema hivyo isipokuwa watu wengi huwa hawaelewi au
wanawake wengi huwa hawaelewi kama mimba zao zimeharibika kwani hutoka
au huaribika kabla wao hawajagundua kama walikuwa wajawazito.
Isipokuwa wale ambao hujua kwamba walikuwa na ujauzito na umetoka hao
wanaweza kuwa asilimia 10 hadi 20, na hizo asilimia zinazobaki kama 35
ni kwa wale ambao hawajui kama mimba zao zimeharibika au walikuwa
wajawazito.
Kwa maana hiyo basi wewe ambaye unatafuta ujauzito kwa muda mrefu
sasa na umekuwa haupati lakini unakuwa unaandamwa na matatizo ya hedhi
kwa mara kadhaa halafu hedhi inakaa sawa basi kuna uwezekano mkubwa
kwamba mimba zako zimekuwa zikiharibika pasipo wewe kujua.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20. Na dalili hizo ni kama;
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20. Na dalili hizo ni kama;
Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke
mwenye mimba, pale mwanamke anapopata ujauzito basi ni vema kabisa kujua
kwamba hatakiwi kabisa kupata hedhi au kutokwa na damu katika via vyake
vya uzazi, kwa maana hiyo basi wewe mwanamke ambaye umepata ujauzito na
bado unaona damu inatoka kidogokidogo basi ni vema kuwahi mapema kituo
cha afya kabla tatizo halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba
(miscarriage) huwa hakutokei ghafla tu huanza taratibu na dalili yake
kubwa ni hii kutokwa na damu ilihali wewe ni mjamzito.
Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge
mabonge na inakuwa nzito, na wakati mwingine mwanamke anaweza akakumbwa
na kutokwa na damu nyepesi na kabla hajatahamaki, damu ile nzito inaanza
kutoka tena, na hii ni dalili mbaya sana ya kwamba ujauzito wako uko
kwenye hatari zaidi na kuna uwezekano ujauzito ulionao ukatoka, kwa
maana hiyo basi mwanamke anapopatwa na dalili ile ya kwanza ni vema
zaidi kufuata ushauri wa daktari ili kuulinda ujauzito wako.
Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo,
kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado ni changa na unapatwa na maumivu
makali sana ya mgongo au kiuno au vyote kwa pamoja basi ni vema kuwahi
kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi gani unaweza kuzuia ujauzito wako
usitoke au usikumbwe na tatizo hili la kutokwa na ujauzito
(miscarriage).
Kama unapatwa na dalili kama hizi kutokwa na damu nyepesi au nzito
ilihali wewe ni mjamzito basi ni vema kuwahi kituo cha afya au wasiliana
nasi ili kukusaidia.Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye
vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.
Nawatakia afya njema.
Nawatakia afya njema.
Itaendelea wiki ijayo!

إرسال تعليق