TATIZO LA KUHARIBIKA KWA MIMBA (MISCARRIAGE)

Wiki iliyopita tulizungumzia tatizo la kuharibika kwa mimba na tukagusia baadhi ya dalili ambazo zinaweza kumpata mwanamke anayeweza kukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba. Na dalili hizo ni kama;
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba.
Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabongemabonge na inakuwa nzito.
Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo (miscarriage). Wiki iliyopita tuliishia hapo, na sasa wiki hii;
Maumivu makali ya tumbo, wakati mwanamke anapokuwa ni mjamzito lakini wakati huohuo anapatwa na maumivu makali ya tumbo ya mara kwa mara yakiambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kutokwa na damu nyepesi au nzito basi ujue ujauzito wako uko kwenye hatari ya kutoka hivyo ni vizuri ukawasiliana na kituo cha karibu cha afya au ukawasiliana nasi kwa matibabu zaidi.
VYANZO VYA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
Vyanzo vikubwa vya kuharibika kwa mimba ni kama vifuatavyo;
Chromosome Abnormalities, mimba nyingi ambazo huharibika hadi wiki ya ishirini husababishwa na tatizo hili la Chromosomes na Chromosomes huwa zinabeba genes ambazo huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi yake itakuwaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie ndani sana lakini matatizo haya ya Chromosomes huchangia sana kuharibika kwa mimba.
Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke (Infections), kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases (PID) yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au Fangasi nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba.
Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba za mara kwa mara, wanawake au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani huweza kuharibu shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la Miscarriage au kuharibika kwa mimba.
Itaendelea wiki ijayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post