Wakulima wa tumbaku wadhulumiwa bilioni 50/- Tabora

Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wamedhulumiwa zaidi ya Shilingi bilioni 50 za mauzo ya zao hilo , Bunge limeelezwa.


Hayo yalielezwa na Zitto Kabwe (Chadema Kigoma Kaskazini), alipouliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, akitaka tamko la serikali kuhusu upotevu huo wa fedha za wakulima wa tumbaku mkoani Tabora.


Alisema wakulima wamedhulumiwa  Dola milioni 28 sawa na Shilingi bilioni 50 kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Licha ya fedha za  wakulima hao mkoani Tabora, kupotea mwaka jana  hadi  sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na serikali kukabiliana na  upotevu huo.


Naibu Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey  Zambi alikiri kwamba serikali inatambua upotevu wa fedha nyingi za wakulima mkoani Tabora, akithibitishia kuwa taarifa hizo zilipofika wizarani na  hatua zilichukuliwa  kwa kupeleka wakaguzi.


Alisema kwa kuzingatia taarifa ya CAG, suala hilo liliwasilishwa ofisini kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na kwamba linaeandelea kufanyiwa kazi, na lipo katika hatua tofauti za utekelezaji.


“Kilichobainika ni kwamba wizi huu unafanyika maeneo mbalimbali nchini na unashirikisha baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na watumishi wa benki wasio waadilifu,” alieleza Naibu Waziri Zambi.


Katika swali la msingi, Rukia Kassim Ahmed (Viti Maalum), alitaka kufahamu ikiwa serikali imefanya utafiti wa kina juu ya faida na hasara inayopatikana kwenye tumbaku.


Kadhalika alihoji endapo serikali  ipo tayari kuwasaidia wakulima wa zao hilo, kupata mbadala wa tumbaku ili kuepusha madhara kwa afya zao.

Zambi alisema zao hilo pamoja na kusaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya pato la taifa ambapo mwaka jana, liliongoza kuleta fedha za kigeni

Post a Comment

Previous Post Next Post