Serikali imepiga marufuku kuchapishwa na kusambazwa kwa gazeti la kila wiki la The EastAfrican kwa madai ya kuwa halijasajiliwa nchini humo.
Hata hivyo Wilfred Kiboro, mwenyekiti wa kampuni ya
Nation Media Group, wachapishaji wa gazeti hilo la lugha ya kiingereza,
ameeleza kuwa adhabu hiyo haikutarajiwa na wala haistahili na kubainisha kuwa
wamekuwa wakisambaza gazeti hilo kwa miaka 20 bila matatizo.
Kampuni ya Nation imedai sababu kubwa huenda ni serikali
ya kutofurahishwa na msimamo wake wa kuandika habari dhidi ya maovu kama rushwa
na kero nyingine nchini.
Kampuni hiyo imesema serikali imetaja kutofurahishwa na kibonzo kilichochapishwa katika toleo la wiki hii, ambapo imesema kimemdhalilisha Rais Jakaya Kikwete
.jpg)
إرسال تعليق