Unyama wa kutisha! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina la Feromena, mkazi wa Meko-Mtongani, Kunduchi jijini Dar, anatuhumiwa kumcharanga viwembe mwanaye wa kumzaa aliyetajwa kwa jina moja la Zena mwenye umri wa miaka kumi.
Mtoto anayefahamika kwa jina la Zena anayedai kunyanyaswa na mama yake.
Tukio hilo la kulaaniwa lilijiri Jumanne wiki hii nyumbani kwa
mwanamke huyo maeneo hayo ambapo mama huyo inadaiwa alimsulubu mwanaye
huyo anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Mtakuja.
Sehemu ya majeraha ya viwembe kichwani kwa mtoto Zena.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mama huyo alidaiwa kumfungia
ndani mwanaye huyo na kuanza kumpa kipigo cha mbwa mwizi.Walidai kwamba
ukiachana na siku hiyo, mama huyo amekuwa akimsulubu mwanaye huyo mara
kwa mara kwa kumcharanga viwembe na vitu vyenye ncha kali hivyo
kumwachia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.
Sehemu ya majeraha yaliyo mgongoni mwa zena.
Mjumbe wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Mziga
alikiri kupokea malalamiko kutoka kwa majirani juu ya unyanyasaji na
uteswaji wa mtoto Zena.Mjumbe huyo alisema kuwa tuhuma hizo
alishazifikisha polisi ambapo mama huyo alikamatwa lakini baada ya muda
alionekana akidunda mtaani kama kawa.
Mama mzazi wa mtoto Zena,Bi.Feromena akibanwa kwa maswali.
Baada kujazwa habari na majirani na mjumbe huyo, kile kikosi kazi cha
Oparesheni Fichua Maovu cha Global Publishers kiliingia mzigoni ambapo
kilianza kwa kumsaka mtoto huyo na kuzungumza naye.Alipopatikana, mtoto Zena alieleza namna mama yake alivyokuwa akimfanyia matendo ya kinyama huku akimnyima haki ya msingi ya kwenda shule.
Mama Zena, Bi. Feromena akiwa chini ya ulinzi.
Alisema mama yake amekuwa akimtuhumu kumwibia fedha zake na kwenda
kutumia shuleni hivyo hakupaswa kurudi tena shuleni na kuongeza kuwa
siku ambazo alikuwa akilala kwa amani ni zile ambazo alikuwa ametoroka
nyumbani na kwenda kulala kwa majirani.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo wa kusikitisha.
OFM ilishuhudia mwili wa Zena ukiwa na makovu na kuvimba huku akidai
kuwa aliunguzwa na ‘frampeni’ (kikaangio) hasa sehemu za kiunoni na
mgongoni.Alisema mama yake alimtishia kuwa endapo atamwambia baba yake
atakiona cha mtema kuni.“Jamani mama amekuwa akinipiga na kunikata viwembe bila kuniambia kosa langu. Naombeni msaada nateseka,” alisema Zena kwa masikitiko makubwa.OFM, kwa kwa kushirikiana na mjumbe wa eneo hilo walikwenda kuripoti tukio hilo kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mtongani lakini hakukuwa na dawati la jinsia hivyo polisi walikwenda kumkamata mama huyo kwa ajili ya kumpeleka kituo kikubwa.
Moja ya wazee akionesha jalada la kesi aliyofunguliwa mama zena.
Kwa upande wake mama huyo alipoulizwa sababu hasa ya kumsulubu
mwanaye alisema si kweli bali anachojua ni siku moja aliyompiga baada ya
kuchukua fedha zake na kwenda kununulia maandazi.“Sijui aliyemkatakata viwembe,” alisema mama Zena kwa kifupi.
Baada ya kufikishwa kwenye kituo kikubwa cha Polisi cha Kawe, mama huyo alifunguliwa jalada la kesi namba KW/RB/439/015-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI hivyo anasubiri kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
إرسال تعليق