Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson
Mwakyembe amesema watamaliza kipindi chao utawala wa awamu ya nne kwa
kuimarisha usafiri wa Reli ya Kati uliokuwa ‘umekufa’ kwa muda mrefu.
Dk Mwakyembe aliyasema hayo Dar es Salaam juzi
usiku katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha
Televisheni cha ITV.
Alisema licha ya sekta ya reli kukabiliwa na
changamoto mbalimbali, wizara yake imeendelea kuboresha sekta hiyo,
ikiwamo kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaohujumu fedha za
umma.
Dk Mwakyembe alisema tangu Serikali imtimue
mwekezaji njia ya Reli ya Kati, ambayo ni Kampuni ya India ya Rites,
mwelekeo uliopo ni kuhakikisha usafirishaji unaongezeka kwa tani za
mizigo na abiria njia zote za reli nchini.
“Kabla ya mwekezaji tulikuwa na uwezo wa kubeba
tani milioni 1.5 na tulikuwa tunafikiria kwenda hadi tani milioni 5,
lakini mwekezaji huyo alipoingia uzalishaji ukaanza kushuka tani 900,000
mara 500,000,” alisema.
“Kinachosikitisha zaidi, mpaka tulifikia
usafirishaji wa tani 190,000 kwa mwaka, tukaona hapana wacha atupishe
ili tuanzishe harakati zetu wenyewe.”
Dk Mwakyembe aliwaonya watumishi wabadhirifu, akisema hawatakuwa na nafasi ya kuendelea na ubadhirifu wao.
“Kwa mfano, udhaifu uliojitokeza kwenye ununuzi
mabehewa, nasubiri uchunguzi wa kamati, hatuwezi kuwatuma watu kazi,
halafu wanakwenda kupima suti India,” alisema.
Kuhusu viwanja vya ndege, alisema kwa sasa wizara
yake iko kwenye mpango wa kukarabati viwanja vikubwa vya ndege mikoani
kabla ya kununua ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Post a Comment