'Tutazidisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya'

Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa.
Kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya nchini kimesema kitazidisha nguvu katika kupambana kuwadhibiti wafanyabiashara wakubwa wa  dawa hizo, waingizaji  na watumiaji.
 
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa, wakati akihojiwa na kuhusu mikakatika ya kikosi chake ya kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya na watumiaji.
 
Alisema wamegundua mbinu ambazo zinatumiwa na wafanya biashara wa dawa hizo kuziingiza nchini na kwamba kikosi chake kimejipanga kikamilifu kukabiliana nao.
 
 “Tumejipanga vizuri kwenye mipaka yote, baharini hata kwa wale wanaotumia magari kusafirishia dawa hizo kwani hivi sasa wafanyabiashara hawa wamekuja na mbinu nyingi kama za kuficha madawa hayo kwenye mabomba ya gesi, simtank, samaki wabichi huku wengine wakibeba kwenye mikasi ya kukatia michongoma,” alisema Nzowa.
 
Alisema dawa zinazoingizwa nchini kwa wingi nchini ni Cocain na Heroin na njia  wanazotumia ni bahari na kulifanya Jiji la  Dar es Saalam kuongoza kwa uingizaji wa dawa hizo likifuatiwa na Tanga kisha Lindi.
 
Kutokana na malalamiko ya watu wengi wakidai kuwa wanaokamatwa ni watumiaji tu huku wakiwaacha wafanyabiasha wanaowatuma, Nzowa alisema hakuna atakayesalimika kwani hadi sasa wamekamata robo tatu ya wafanyabiashara wakubwa na kesi zao zipo mahakamani

Post a Comment

Previous Post Next Post