Kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya nchini
kimesema kitazidisha nguvu katika kupambana kuwadhibiti wafanyabiashara
wakubwa wa dawa hizo, waingizaji na watumiaji.
Kutokana na malalamiko ya watu wengi wakidai kuwa wanaokamatwa ni
watumiaji tu huku wakiwaacha wafanyabiasha wanaowatuma, Nzowa alisema
hakuna atakayesalimika kwani hadi sasa wamekamata robo tatu ya
wafanyabiashara wakubwa na kesi zao zipo mahakamani
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa,
wakati akihojiwa na kuhusu mikakatika ya kikosi chake ya kupambana na
wafanyabiashara wa dawa za kulevya na watumiaji.
Alisema wamegundua mbinu ambazo zinatumiwa na wafanya biashara wa
dawa hizo kuziingiza nchini na kwamba kikosi chake kimejipanga
kikamilifu kukabiliana nao.
“Tumejipanga vizuri kwenye mipaka yote, baharini hata kwa wale
wanaotumia magari kusafirishia dawa hizo kwani hivi sasa wafanyabiashara
hawa wamekuja na mbinu nyingi kama za kuficha madawa hayo kwenye
mabomba ya gesi, simtank, samaki wabichi huku wengine wakibeba kwenye
mikasi ya kukatia michongoma,” alisema Nzowa.
Alisema dawa zinazoingizwa nchini kwa wingi nchini ni Cocain na
Heroin na njia wanazotumia ni bahari na kulifanya Jiji la Dar es
Saalam kuongoza kwa uingizaji wa dawa hizo likifuatiwa na Tanga kisha
Lindi.

إرسال تعليق