Wanakuja kwa makundi. Wake kwa waume, vijana kwa wazee, wenye
elimu na historia tofauti za kimaisha... lakini kilichowaleta China,
Hong Kong na Macau ni kimoja tu; biashara ya dawa za kulevya.
Hawa ni zaidi ya Watanzania 130 ambao wamefungwa katika magereza mbalimbali kwenye nchi za China, Hong Kong na Macau.
Ingawa wanadai kupata mlo mzuri, mahali pazuri pa
kulala na fursa kadhaa katika magereza, lakini bado wamekosa kitu kimoja
muhimu duniani; uhuru.
Faraja wanayoitegemea ni ya Mchungaji John
Wootherspoon, raia wa Australia anayeishi China ambaye amepata kibali
cha kutembelea magereza mbalimbali.
Wafungwa wa Kitanzania wapo katika magereza mbalimbali kama Shek Pik, Stanley, Loo Woo na Macau.
Fursa ya kukutana na wafungwa ilikuwa ndicho
chanzo cha Wootherspoon kuona kuwa kuna idadi kubwa ya Watanzania katika
magereza kuliko hata idadi ya wazawa wenyewe.
“Kila mwezi Watanzania wanne hadi sita walikuwa
wakiingia magerezani na wengine wengi wakiwa rumande kwa makosa
mbalimbali,” anasema
Wootherspoon ana kazi moja kubwa katika magereza hayo, ambayo ni kuwafariji kwa neno la Mungu.
“Ninapata nafasi ya kukaa nao kila siku na
ninapowasikiliza, nimegundua kuwa wanajuta na wametumiwa tu na watu
wenye ufahamu na biashara hiyo,” anasema
Wootherspoon, ambaye yupo nchini kwa sasa, anasema
kuwa anachotaka ni kuwakataza vijana wengine kwenda China kwa
kusafirisha dawa za kulevya.
Ujumbe wa majonzi kwa ndugu za
wafungwa
= Soma Zaidi Mwananchi
= Soma Zaidi Mwananchi
إرسال تعليق