Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), vimetangaza mgogoro dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Moshi Vijijini, Fulgence Mponji, anayedaiwa kutumia nafasi yake
kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumuapisha mgombea aliyeangushwa
katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nduoni,
Kilichopo Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Hemed Msabaha, alisema Ukawa imetoa siku saba kwa mkurugenzi huyo kufuta kiapo alichokitoa kwa mgombea wa CCM na badala yake atende haki kwa kumwapisha mshindi halali, Thomas Ngowi (NCCR), aliyechaguliwa kwa kura 163 dhidi ya Joseph Msaki (CCM) aliyepata kura 158 na Richard Msaki (TLP) aliyeambulia kura tisa.
“Hatupo tayari kuona haki yetu inaporwa kihuni, tunataka mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi ule, afute kiapo batili alichofanya kwa minajili ya kukibeba CCM. Tunampa siku saba za kushughulikia mgogoro huu, kabla nguvu ya umma haijazuia ofisi ya kijiji kufunguliwa, lakini pia kuanza maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza Mponji ajiuzulu,” alisema Msabaha.
Alisema sababu za kutangaza mgogoro huo inatokana na mkurugenzi huyo kutangaza NCCR wameshinda vijiji 27 sawa na asilimia 17, lakini likafanya kosa la jinai kwa kuwaapisha wenyeviti 26 tu na kumwapisha isivyo halali, mgombea wa CCM badala ya NCCR aliyetangazwa mshindi.
Hata hivyo, mshindi wa nafasi hiyo, Thomas Ngowi (NCCR), aliiambia NIPASHE kuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Emilly Kessy, alimtangaza mshindi baada ya kuwashinda wapinzani wake, lakini Jumanne alipewa taarifa kuwa mpinzani wake Joseph alishaapishwa na mkurugenzi huyo.
Kwa mujibu wa fomu ya matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti, yenye namba IX iliyotolewa chini ya kanuni ya 25 (I) na 23 (3) ya chaguzi za serikali za vijiji, ikasainiwa na msimamizi huyo na baadaye kugongwa muhuri wa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nduoni, (NIPASHE imeona nakala yake), inaeleza mshindi wa uchaguzi huo ni Thomas Ngowi.
Katibu wa Chadema, Jimbo la Vunjo, Emanuel Mlaki, alisema kitendo kilichofanywa na mkurugenzi huyo hakikubaliki na hakina uhalali wa kisheria wa kubadilisha mshindi wa uchaguzi huo na kumpa ushindi mgombea wa chama tawala ili kujilinda asitimuliwe katika nafasi yake ya ukurugenzi.
Mkurugenzi huyo (Mponji), alikana kuwa kwa nafasi yake kama msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya, yeye hakutangaza matokeo ya uchaguzi huo, kijiji cha Nduoni bali aliyetangaza ni msimamizi wa uchaguzi aliyeko kwenye kituo hicho.
“Sitangazi matokeo, mimi natoa taarifa. Ila mimi nililetewa matokeo na msimamizi wangu niliyemteua kwa barua na aliyoniletea ndiyo yapo kwenye taarifa yangu na wala sipokei matokeo kutoka kwa mtu mwingine yeyote…kama wanaona hawakuridhika wakatafute haki yao mahakamani,” alisema.

CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment