Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya
Congo wamekubali mswada ambao wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais
Joseph Kabila idhini ya kubaki madarakani, baada muhula wake wa pili
kumalizika.
Mswada huo unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla
ya uchaguzi ambayo serikali inasema inaweza kuchukua miaka kadha
kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu.
Mwandishi
wa BBC mjini Kinshasa anasema wabunge wengi wa upinzani walisusia kura
hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba
Post a Comment