Askari jeshi wanaodhaniwa kuwa
wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka watu zaidi ya 60 katika
nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana miongoni mwa
mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi mbili hizo.Na
inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji wa tukio
hilo.
Boko Haram siku za hivi karibuni zimekamata udhibiti wa miji
kadhaa na vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na sasa
wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani wanazopakana na Nigeria .Katika
shambulio hilo la siku ya Jumapili askari hao walivamia vijiji viwili
vilivyoko eneo la Tourou .
Katika uvamizi huo nyumba kadhaa
zilichomwa moto na idadi ya mateka ni themanini kati yao watu wazima ni
thelathini,na watoto wapatao hamsini na walielekea upande wa Kaskazini
mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo.
Cameroon imekuwa ikiishutumu Nigeria kwa kushindwa kufanya juhudi za ziada za kukabiliana na kundi hilo la Boko Haram
Post a Comment