Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya
umefungwa leo kwa masaa kadhaa baada ya ndege moja kulazimika kutua kwa
tumbo kutokana na matairi yake kushindwa kufunguka.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA)
Maafisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya wamesema kuwa, shughuli
za usafiri katika uwanja huo zimezorota kwa zaidi ya masaa matano na
ndege zote zikalazimika kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mombasa.
Ndege hiyo ya ndani ilikwama kwenye barabara ya kutua ndege baada ya
kusimama kikamilifu. Hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusiana na ajali
hiyo.
Wakati huo huo maafisa usalama wa Kenya wameanza kufanya uchunguzi
kuhusiana na kifo cha Fidel Odinga, mwana wa Waziri Mkuu wa zamani wa
nchi hiyo Raila Odinga, ambaye amekufa leo asubuhi.
Wakati huo huo salamu za rambirambi zimeendelea kumiminika nyumbani kwa
Raila Odinga ambaye ni mkuu wa mrengo wa upinzani wa Cord.
Katika upande mwingine, shahidi mmoja aliyetoa ushahidi kwenye Makahama
ya Kimataifa ya Jinai ICC amepatikana ameuawa huku mwili wake ukiwa una
viungo pungufu.
Vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti leo Jumapili kuwa, mwili wa
Meshak Yebei ulipatikana siku ya Ijumaa baada ya kutoweka kwa muda wa
wiki nzima nyumbani kwao, katika Kaundi ya Uasin Gishu, jambo ambalo
limezusha wasiwasi kati ya watu wa familia na wanaharakati wa haki za
binadamu.
Mwili wa Yebei ulipatikana unaelea kwenye Mto Yala katika Kaunti ya
Nandi, zaidi ya kilomita 40 kutokana nyumbani kwake huko Sugoi, katika
Kaunti ya Uasin Gishu.
Source: kiswahili.irib.ir
Post a Comment