Makabiliano
makali yametokea kati ya waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya
usalama katika ikulu ya Rais ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu
ya Rais.
Walioshuhudia makabiliano hayo wanasema waasi hao
walipambana na vikosi vya usalama kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu
ya Rais.
Awali, Rais Abd Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo
ya dharura na washauri wake siku moja baada ya vifo vya watu tisa
kufuatia makabiliano mengine kati ya waasi hao na wanajeshi mnamo
Jumatatu.
Makubaliano yalifikiwa lakini waasi wa Houthis waliendelea kuzingira ikulu ya Rais na makao ya waziri mkuu.
Kiongozi
wa waasi hao anatarajiwa kutoa hotuba baadaye leo wakati baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kwa mkutano wa dharura kujadili
hali nchini Yemen.
Kanali Saleh al-Jamalani, ambaye ni mkuu wa
kikosi cha ulinzi wa ikulu ya Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, ameambia
sjirika la habari la AP kwamba waasi haowalivamia ikulu nyakti za
mchana.
Rais Hadi inaarufiwa hakuwa katika makao hayo wakati waasi walioivamia ikulu.
إرسال تعليق