Wafanyabiashara wa mifugo wagoma kuchinja mifugo yao na kufunga mabucha bukoba.

Wafanyabiashara wa mifugoa mjini bukoba wamegoma kuchinja mifugo yao na kutofungua mabucha wakilalamikia kuamrishwa   na serikali  kupunguza bei ya nyama  kutoka shilingi elfu tano had elfu nne  kwa kilo.
Wakiongea katika machinjio ya rwamishenye mjini bukoba wafanyabiashara hao wasema wamegoma kuchinja mifugo hiyo na kutofungua mabucha  kabisa  kutokana na barua  waliyopewa  kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya  manispaa ya bukoba yakuwata kupunguza bei ya nyama   hali ambayo imepelekea wafanyabiashara kususia barua hiyo na kugoma kuchinja mifugoa yao.
 
Kwaupande wake  mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Haji Yatubu Musa  amesema   wao hawawezi kuchinja mifugo hiyo kutokana na na changamoto  mbalimbali wanazo kabiliana nazo katika kununua mifugo hiyo  na kuisafirisha  ambapo amezitaka mamlaka husika kuangali upya suala hili na kulitafutia ufumbuzi.
 
ITV imemtafuta mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya manispaa ya bukoba Chibunu Lukiku ambapo amekataa  kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari na kudai kwamba leo sio siku ya kazi   nakudai kuwa yeye sio mchinjaji wa mifugo hiyo.
 
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya bukoba Siporah Pangani  amesema    nikweli wafanyabiashara hao walipelekewa barua ya kubunguza bei ya nyama kwakuwa walipandisha bei kiholela bila kibali kutoka kwenye mamlaka husika  hali ambayo imepelekea usumbufu kwa  wananchi wa mkoa huo
- itv

Post a Comment

Previous Post Next Post