Wafanyabiashara wa mifugoa mjini bukoba wamegoma kuchinja mifugo yao
na kutofungua mabucha wakilalamikia kuamrishwa na serikali kupunguza
bei ya nyama kutoka shilingi elfu tano had elfu nne kwa kilo.
Wakiongea katika machinjio ya rwamishenye mjini bukoba
wafanyabiashara hao wasema wamegoma kuchinja mifugo hiyo na kutofungua
mabucha kabisa kutokana na barua waliyopewa kutoka kwa mkurugenzi wa
halmashauri ya manispaa ya bukoba yakuwata kupunguza bei ya nyama
hali ambayo imepelekea wafanyabiashara kususia barua hiyo na kugoma
kuchinja mifugoa yao.
Kwaupande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Haji Yatubu Musa
amesema wao hawawezi kuchinja mifugo hiyo kutokana na na changamoto
mbalimbali wanazo kabiliana nazo katika kununua mifugo hiyo na
kuisafirisha ambapo amezitaka mamlaka husika kuangali upya suala hili
na kulitafutia ufumbuzi.
ITV imemtafuta mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya
bukoba Chibunu Lukiku ambapo amekataa kutoa ushirikiano kwa waandishi
wa habari na kudai kwamba leo sio siku ya kazi nakudai kuwa yeye sio
mchinjaji wa mifugo hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya bukoba Siporah
Pangani amesema nikweli wafanyabiashara hao walipelekewa barua ya
kubunguza bei ya nyama kwakuwa walipandisha bei kiholela bila kibali
kutoka kwenye mamlaka husika hali ambayo imepelekea usumbufu kwa
wananchi wa mkoa huo
- itv

إرسال تعليق